2014-07-17 15:44:03

Mtu kwao!


Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Argentina walioshiriki kwenye mashindano ya Kombe la Dunia nchini Brazil kwa mwaka 2014 wamemzawadia Baba Mtakatifu Francisko jezi iliyopambwa kwa sahihi za wachezaji kutoka Argentina. Wachezaji hawa kutoka Argentina hata baada ya kuchalazwa bao moja kwa nunge na Wajerumani, wanamshukuru Baba Mtakatifu Francisko kwa kuwakumbuka na kuwaombea walipokuwa wanashiriki katika mashindano ya Kombe la Dunia, huko Brazil.

Picha kubwa ya Baba Mtakatifu akiwa na wachezaji wa timu ya taifa ya Argentina ilipambwa katika eneo ambalo wanamichezo hawa walikuwa wanafanyia mazoezi yao nchini Brazil. Hii ni picha waliyopiga na Baba Mtakatifu wakati walipomtembelea mjini Vatican hivi karibuni.







All the contents on this site are copyrighted ©.