2014-07-15 12:02:37

Monsinyo Wojciech Zaluski ateuliwa kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Burundi


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Monsinyo Wojciech Zaluski kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Burundi na kumpandisha hadhi ya kuwa ni Askofu mkuu. Monsinyo Zaluski kabla ya uteuzi huu alikuwa ni mshauri katika Ubalozi wa Vatican nchini Guatemala.

Askofu mkuu mteule Zaluski alizaliwa kunako tarehe 5 Aprili 1960. Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi, akapadrishwa kunako mwaka 1985 na tangu wakati huo, akajiunga na Taasisi ya Kipapa Diplomasia pamoja na kuendelea na masomo yake ya Sheria za Kanisa kwenye Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregoriana na hapo akajipatia shahada ya uzamivu.

Baada ya masomo yake, mwaka 1989 akaanza kutoa huduma kwenye Balozi za Vatican kama Katibu mkuu wa Balozi huko: Burundi (1989 - 1991), Malta (1991 - 1994), Albania (1994 - 1996), Zambia (1996 - 1997), Sri Lanka (1997- 2000), Georgia (2000 - 2003), Ucrain (2003 - 2006) na Ufilippini (2006 - 2010). Kunako mwaka 2010 akateuliwa kuwa ni mshauri wa Ubalozi wa Vatican nchini Guatemala.







All the contents on this site are copyrighted ©.