Jumapili hii ni Siku ya watu wanaoishi na kufanya kazi katika maeneo ya bahari.
Kwa ajili hiyo, Kardinali Antonio Maria Vegliò, Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili
ya wakimbizi, wahamiaji na Watu wanaohamahama, akihojiwa na Mwanahabari Mario Ponzi
, amesema pamoja na kero nyingi zinazofanyika katika ulimwengu wa bahari, hakuna hata
mmoja anayeweza kutengwa katika Kazi za kichungaji za Kanisa. Alitaja baadhi keoro
zinazosumbua kuwa ni uharamia kwa usafiri wa watu na bidhaa majini, kukataliwa kwa
makazi ya Wagypsy, utalii kama injini ya maendeleo ya binadamu, pamoja na mengine
yanayofanyika katika ulimwengu huu wa Bahari.
Na Kardinali Veglio, alieleza
kuwa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Kazi za Kichungaji kwa Wakimbizi , watalii na
watu wasiokuwa na makazi maalum kama Mabaharia na wavuvi katika Ulimwengu wa Bahari,
kwa njia ya mikutano ya kimataifa, na upelekaji wa ujumbe wake na ufadhili , linaendelea
kuzingatia tahadhari ya dunia juu ya mambo haya yanayoathiri watu.
Pamoja
na kuzungumzia watu wa bahari, lakini pia mawazo yake aliyapeleka kwa watu wanaoishi
mitaani , na pia juu ya wa siku kujitolea na siku ya utalii, katika nyanja chanya
na hasi. Na kwamba . ulimwengu wa mabaharia, kwa wengi haujulikani ingawa kuna kundi
kubwa la binadamu wapatao zaidi ya milioni moja wanaoishi katika ulimwengu wa maji,
wakiwemo mamia ya maelfu ya Mabaharia na Manahodha wa meli wanaosafiri kila siku
katika ulimwengu wa bahari. Hivo Kanisa haliwezi kupuuza dunia hii inayoishi mbali
na upeo wa macho ya wanaoishi nchi kavu au kupuuzwa na jamii kwa ujumla, wakati
wakipita katika bandarini.
Madhumuni ya kuwa na Siku ya ulimwengu wa Bahari
ambayo hufanyika kila mwaka 13 Julai, katika mzunguko wa Kanisa Katoliki, lakini
pia kwa madhehebu mengine ya kikristo, ni kuongeza uelewa kuhusu umuhimu wa kazi iliyofanywa
na inayoendelea kufanywa na mabaharia katika maisha ya binadamu kila siku. Kardinali
amelitaja hili kuwa ni deni kwa watu wanaoishi nchi kavu, kwa sababu hutegemea mengi
kutoka sekta ya bahari, ikiwemo usambazaji wa chakula na bidhaa kwa ajili ya matumizi
yetu ya kila siku.
Kardinali Veglia pia alirejea hatari zinazokabili taaluma
ya duniani hii, na kukiri kwamba, kuna matatizo mengi na hatari mbele ya uso wao
kila siku, na hata kama inaonekana, na hasa hatari inayoonekana kuwa kubwa leo hii
ni uharamia, kama taarifa zinavyosikika toka hapa na pale, hasa utekwaji nyra wa vyombo
vya majini kwa madai ya kulipwa fidia kama ilivyosikika katika bahari ya Ghuba ya
Aden. Ingawa sasa katika eneo hilo, tatizo limepungua baada ya kuwepo walinzi wenye
silaha kali lakini bado hapajawa salama kabisa.
Katika miezi ya karibuni
kumeanza tena baadhi kumekuwa na vurugu katika Ghuba ya Guinea, na katika ukanda
wa Malacca na katika bandari nyingi za Amerika ya Kusini. Katika hili , utume wa
Kanisa kwa wakazi wa Bahari hutoa ujumbe wa amani na matumaini katika nguvu ya Mungu
na majitolea ya nguvu ya mshikamano katika utoaji wa msaada wa kiroho si tu kwa waathirika
wa uharamia baharini , lakini pia kwa familia zao, kuwafariji katika yote maumivu
ya kisaikolojia na kiroho na matokeo yake.