Tangu Ijumaa katika ukumbi wa Casina Pio IV,wa hapa Vatican , kumekuwa na warsha
ya Kimataifa ya siku mbili 11-12 Julai , iliofanyika katika mazingira ya faragha,
kama ilivyoandaliwa na Baraza la Kipapa a Haki na Amani na Sekretarieti ya Nchi,
juu ya haki katika manufaa ya dunia, kuelekea uchumi shirikishi katika ngazi ya kimataifa
na mshikamano wenye umoja zaidi ,katika uchumi .
Mkutano ulihudhuriwa na
wasomi Sabini, wawakilishi wa biashara kubwa na vyama vya kiraia, kama ilivyoandaliwa
na kupangwa kwa kushirikiana na taasisi za kimataifa, ikiwemo Benki ya Dunia, Shirika
la Ushirikiano wa Kiuchumi Maendeleo (OECD / OSCE), Mkutano wa Umoja wa Mataifa juu
ya Biashara na Maendeleo (UNCTAD),na mashirika mengine IMF, FAO, ILO. Madhumuni
ya mkutano ni kuimarisha mtazamo uliotajwa na Papa Francisco, katika waraka wake
wa Kitume, wenye jina “Evangelii Gaudium"Furaha ya Injili : kwamba ni muhimu daima
mipango ya uchumi kuwashirikisha wote.
Majumuisho ya agenda za majadiliano
yanaelezea semina, hasa ililenga kuchambua maelezo msingi ya Papa Francisco katika
waraka wake wa Injili ya Furaha, katika masuala ya uchumi, ambamo ametaja misingi
ya kuheshimu utu wa binadamu na uungaji mkono juhudi zote zinazolenga kutetea haki
na uvumilivu ili kwamba, hakuna uchumi wa kutengana. Ni kuondokana na hali ya sasa
ambamo binadamu anachukuliwa kama ni bidhaa za kutumika na kutupwa!. Papa ameonya
kwamba kizazi cha leo, kimetengeneza utamaduni wa kutupa , ulioenea kote. Si tena
suala jepesi la uwepo wa unyonyaji na ugandamizaji, lakini mfumo mpya wa aina yake.
Waraka unaendelea kuonya dhidi ya utengano wa kimbinu katika mifumo muhimu
ya maisha ya kijamii, ambamo kila njia ya kujiinua kwa watu maskini, imezibwa kiujanja
na wale waliotangulia na, na hivyo hakuna tena sehemu Maskini wanapoweza kujiinua
isipokuwa kwa huruma ya mabwanyenyena mabepari .
Pamoja na onyo hilo, Papa
hakusahau kuwataja wale wanaofanya vyema, baadhi ya viongozi wa makampuni makubwa
na wafanya biashara, ambao hutoa mchango mkubwa fedha na majitoleo binafsi kwa ajili
ya kufanikisha maendeleo ya binadamu katika karne hii. Na Papa anataja uwepo wa
baadhi ya viongozi wa uchumi duniani wanaoonyesha nia na ubunifu kwa ajili ya kuboresha
maisha ya watu wengi katika na ukweli wao kama watalaam .
Hivyo kupitia semina
hii , Baba Mtakatifu alitegemea washiriki watachambua kwa kina jinsi gani uchumi unaweza
kupanua faida zake na kupunguza matundu mabaya na hali mbaya za uchumi. Kama alivyosema
mapema mwaka huu ,Fedha na biashara ya kimataifa inaweza kuchangia zaidi katika uwekezaji
wa ujuzi kwenye huduma ya walio badokatika hali mbaya ya umasikini. Hivyo Semina
ililenga kujadili mambo haya na kupendekeza njia zinazoweza kufaa zaidi katika kuinua
ukuaji wa uchumi kwa watu wote . Hivyo kwa njia ya semina hii, Baraza la Kipapa
kwa ajili ya haki na amani,, nalo linategemea kupata ufahamu wa ziada na msaada katika
kuelewa vizuri zaidi jinsi ya kuboresha mambo mengi ya binadamu ndani ya uchumi wa
utandawazi na kuwezesha watu wanaokadiriwa kufikia milioni mbili kutoka katika umaskini
wa kukithiri.