2014-07-10 10:28:15

Papa Francisko ataka mabadiliko ya haraka katika Idara ya uchumi Vatican


Kardinali George Pell, Mkuu wa Sekretarieti ya Uchumi ya Jimbo Takatifu, anasema , kuna changamoto nyingi na kazi nyingi za kufanya kwa ajili ya ufanikishaji wa mabadiliko katika Idara ya Uchumi ya Jimbo Takatifu, hilo alilieleza, Jumatano asubuhi , wakati akikutana na wanahabari katika Ofisi za Vatican, baada ya Taasisi ya Fedha ya Vatican kutoa taarifa yake. Kardinali alitangaza jitihada kubwa zinazo takiwa kushughulikiwa kwa haraka, katika sekta ya APSA (Utawala wa urithi mali za Jimbo la Papa, ), Mfuko wa Pensheni, Mawasiliano na IOR (Taassi ya Benki ), chini ya Uongozi wa Rais mpya Jean -Baptiste de Franssu.

Katika Mkutano huu wa wanabahari , Rais wa IOR aliyemaliza muda wake, , Ernst von Freyberg, aliwaambia wanahabri kwamba, Papa Francisco anapenda kuona mabadiliko ya haraka. Na Kardinali Pell, ameahidi kushughulikia mapungufu na mianya ya hatari katika kuvujisha fedha , iliyotajwa na Tume ya Kipapa, iliyofanya utafiti na kushughulikiwa shirika kiuchumi la utawala wa Kiti Kitakatifu Cosea). Kwa ajili hii, iliundwa Ofisi ya Usimamizi, iliyoongozwa na Danny Casey raia wa Australia Meneja wa zamani wa Biashara jimbo Kuu la Sydney.

Kwa ajili ya mambo ya kawaida kwa urithi wa mali ya Vatican (APSA) inayohamishika ,Jumatano kulichapishwa barua Binafsi “ Motu Proprio ya Papa, inayoamrisha Sekretarieti ya Uchumi, kusimamia mashirika ya Jimbo la Papa, sera na taratibu kwa ajili ya ununuzi na usambazaji wa rasilimali watu. Wafanyakazi wa APSA, watashughulikia zaidi masuala ya hazina, uimarishaji na uanzishaji wa uhusiano wa karibu na benki kuu zote kuu - kama inavyotakiwa na MONEYVAL - kuhakikisha utulivu wa fedha na ulipaji wa madeni kwa Jimbo Takatifu.

Kuhusu Mfuko wa Pensheni, imeteuliwa kamati ya watalaam wakiongozwa na Monsinyori Brian Ferme, akisaidiwa na wajumbe wanne wataalam Kotanko Bernhard (Austria), Andrea Lesca (Italia), Antoine de Salins (France), Prof. Nino Savelli (Italia) kulingana na muundo wa marekebisho yaliyo pendekezwa katika kwa Baraza la Uchumi 2014 kw alengo la kuhakikisha pensheni kwa sasa na kizazi kijacho ni salama zaidi.

Pia kutakuwa na marekebisho katika Idara ya Mawasiliano Vatican, kulingana na mwenendo mpya wa matumizi, na uboreshaji wa uratibu na kupunguza gharama. Ndani ya miezi 12, kamati ya wataalamu wa kimataifa na wawakilishi wa Vatican itatoa mapendekezo yake katika mpango huu , chini ya uenyekiti wa Bwana Christopher Patten a Uingereza , huku akiwa amezungukwa na Gregory Erlandson (USA), Daniela Frank (Ujerumani), p. Eric Salobir (France), Leticia Soberon (Hispania, Mexico) na George Yeo (Singapore). Pamoja na Msgr. Paul Tighe (Kipapa Baraza la Mawasiliano Jamii), James Ghisani (Vatican Radio), Msgr. Carlo Maria Polvani (Katibu wa Jimbo), Msgr. Lucio Adrian Ruiz (Internet Service Vatican) na Giovanni Maria Vian (L'Osservatore Romano).

Hatimaye, usimamizi mpya wa timu ya IOR, wakiongozwa na Jean-Baptiste de Franssu, tangu Jumatano 9 Julai 2014, walianza utekelezaji wa hatua ya Pili ya mabadiliko , baada ya kukamilika kwa hatua ya iliyoongozwa na mtalaam von Freyberg, kwa kutoa vipaumbelevitatu: kuimarisha biashara ya IOR, hoja usimamizi mpya wa urithi wa mali za Vatican na rasilimali(Vam) na shughuli zake zaidi kulenga katika kutoa huduma kwa viongozi wa dini, makanisa, majimbo na walei wafanyakazi wa Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.