Bunge la Ethiopia limepitisha makubaliano yatakayoiwezesha Ethiopia kuisaidia Djbouti
kupambana na ukame unaotishia usalama wa maisha ya watu wengi. Kutokana na makubaliano
haya, Djbouti itaweza kutumia mito ya maji kutoka Ethiopia kwa ajili ya shughuli za
kilimo na umwagiliaji hasa kwenye Bonde la Mto Beluki, hususan kwenye maeneo ya Shinile,
kilometa 100 kutoka mpakani kati ya Ethiopia na Djbouti.
Djbouti inaweza kuvuna
maji ujazo wa mita 103.000 kwa siku kutoka katika mito ya Ethiopia katika kipindi
cha miaka thelathini kuanzia sasa.