2014-07-08 10:48:17

Kardinali Turkson ahudhuria mkutano wa haki na amani (Monaco ya Bavaria)


Kardinali Peter Turkson, Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Haki na Amani, Jumatatu aliuhutubia mkutano na haki, Amani, Maendeleo na Ushirikiano wa kimataifa , ulioandaliwa katika Taasisi Katoliki ya Monaco ya Bavaria. Mkutano huo ulio andaliwa na Taasisi ya Elimu ikishirikiana na Taasisi ya Maarifa na Maendeleo ya Shule ya Falsafa ya Wajeuit, wanaoishi Monaco.

Nia ya kuu ya mkutano huo ni ujenzi wa utamaduni wa haki na Maendeleo yenye manufaa katika utumishi wa kimataifa, kama inavyokuzwa na Taasisi ya Usawa na Uelewa wa mbadala wa dhana ya manufaa ya ulimwengu kwa watu wote, katika mtazamo wa tofauti za kimataifa ya kiutamaduni.

Katika hotuba yake Kardinali aliangalisha katika mchakato mpya ulioanzishwa na Umoja wa Mataifa baada ya MDG, mchakato unaotafuta kuweka malengo mapya ya maendeleo endelevu, yanayo tarajiwa kuonyesha jinsi kujishughulikia dharura na majanga asilia yanayojitokeza na kutafakari juu ya hali ya baadaye ya ajenda ya maendeleo. Katika mchakato huu, ufafanuzi zaidi juu ya umaskini ni jukumu kuu, ikiwa pamoja na haja ya kuunganisha hali ya mazingira katika mjadala wa maendeleo endelevu.Huo, ni pamoja na mgogoro wa kifedha na athari zake, kwa kutafakari muhimu juu ya dhana ya uchumi ya baadaye.

Kardinali aliendelea kueleza kwamba, mgogoro wa kifedha pia kwa mara nyingine unaonyesha kuunganishwa kwa karibu na nguvu ya kutegemeana duniani kote. Kwa hiyo, sasa ni kutafuta ufumbuzi unaoweza hata kama kidogo katika ngazi ya kitaifa au baina ya nchi, lakini ni lazima nchi zote kuzingatia mpango wa taasisi za kimataifa na mshikamano wa jamii yote ya binadamu . Hii ni pamoja na kutafakari juu ya mafanikio na ukuaji wa mifumo kwa siku zijazo.

Kardinali alisisitiza hayo na kusema a ukweli kwamba hakuna tena nchi inayoweza kuamua tu yenye misingi ya kukuza pato lake nchi yake kwa kutegemea utajiri asilia wa nchi nyingine. Alieleza hilo kwa kufanya rejea katika ripoti ya Kamati ya Utafiti ya Ujerumani “Bundestag” juu ya "Kukuza Uchumi, mafanikio, ubora wa maisha, ripoti yake ya mwisho ya kuanzia mwaka 2013 ambayo imehimitimisha kwa kutaja kwamba lengo la ukuaji wa uchumi si kiashiria tosha kwa kijamii kuonyesha zaidi sana ustawi binafsi wa mtu.










All the contents on this site are copyrighted ©.