Maonesho ya Sabasaba, Jijini Dar es Salaam, kumekucha!
Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania amewataka wafanyabiashara nchini kuongeza juhudi za
kuongeza ubora zaidi wa bidhaa zao ili ziweze kushindana na zile za nje ya nchi. Aidha
Rais Kikwete amewapongeza washiriki wa maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa kwa
kuongeza ubora wa bidhaa ambao kila mwaka kumekuwa na tofauti.
Kauli hiyo
imetolewa na Rais Kikwete wakati akitembelea maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa
yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere jijini Dares Salaam, Jumamosi,
tarehe 5 Julai 2014.
“Maonesho ya mwaka huu yamepiga hatua kubwa kwani kumekuwepo
kwa ongezeko la bidhaa, bidhaa zimefungwa vizuri tukiendelea hivi tunaweza kushindana
na bidhaa za kimataifa. Pendekezo langu mimi ni kuendelea kufanya ziwe vizuri zaidi,”
alisema Rais Kikwete.
Akitembelea banda la Jeshi la Magereza, Rais Kikwete
ambapo alijionea uzalishaji wa bidhaa za kilimo na kulitaka jeshil hilo kutoa elimu
kwa wananchi juu ya kilimo bora cha kisasa. Katika ziara hiyo Rais Kikwete alitembelea
mabanda mbalimbali likiwemo la Wakala wa Mafunzo nje ya nchi. Benki Kuu ya Tanzania,
Bidhaa za Tanzaniana mengineyo.