Askofu mkuu Antonio Arcari ateuliwa kuwa Balozi Mpya wa Vatican Costa Ricca
Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Antonio Arcari kua Balozi mpya wa Vatican
nchini Costa Rica. Kabla ya uhamisho huu Askofu mkuu Arcari alikuwa ni Balozi wa Vatican
nchini Msumbiji. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Arcari alizaliwa tarehe 8 Mei 1953
mjini Brescia, Italia.
Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi, akapadrishwa
kunako tarehe 11 Juni 1977. Tarehe 18 Julai 2003 akateuliwa na Baba Mtakatifu Yohane
Paulo wa Pili kuwa Askofu mkuu na Balozi wa Vatican nchini Honduras. Tarehe 12 Desemba
2008 Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto XVI akamteuwa kuwa Balozi wa Vatican nchini
Msumbiji na sasa ameteuliwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Costa Rica.