2014-07-04 09:12:09

Nembo ya Siku ya Vijana Duniani kwa Mwaka 2016


Heri wenye rehema maana hao watapata rehema, ndiyo kauli mbiu itakayoongoza maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani kwa Mwaka 2016 itakayofanyika Jimbo kuu la Cracovia, Poland. Kamati kuu ya maandalizi imechapisha nembo itakayotumika kwa ajili ya maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani ambayo Baba Mtakatifu Francisko anatarajiwa kuhudhuria na kushiriki kikamilifu.

Nembo ina rangi kuu tatu: Bluu, Nyekundu na Njano; inaonesha ramani ya Poland na ndani yake kuna Msalaba inayomwonesha Yesu Kristo, kiini cha mkutano huu. Nembo hii inawaalika vijana kujiaminisha mikononi mwa Mungu, utekelezaji wa maneno ya Mtakatifu Faustina Kowalska aliyeeneza Ibada ya Huruma ya Mungu.

Siku ya Vijana Duniani kwa Mwaka 2016 itaanza kutimua vumbi kuanzia tarehe 26 hadi Julai 2014. Baba Mtakatifu Francisko anatarajiwa kuwasili nchini Poland hapo tarehe 28 Julai 2016.







All the contents on this site are copyrighted ©.