2014-07-02 08:58:42

Askofu mkuu Bernadito C. Auza ateuliwa kuwa ni Mwakilishi wa kudumu wa Vatican Umoja wa Mataifa


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Bernardito C. Auza aliyekuwa Balozi wa Vatican nchini Haiti kuwa Mwakilishi Mpya wa kudumu wa Vatican kwenye Ofisi za Umoja wa Mataifa zilizoko New York, Marekani.

Askofu mkuu Auza anachukua nafasi ya Askofu mkuu Francis Chullikatt, aliyeteuliwa na Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto XVI kunako tarehe 7 Julai na kuanza kutekeleza utume wake kama Mwakilishi wa kudumu wa Vatican kwenye Ofisi za Umoja wa Mataifa kunako tarehe 15 Septemba 2010.







All the contents on this site are copyrighted ©.