2014-07-01 11:26:31

Mauaji ya vijana wa Israeli ni kizingiti cha amani!


Padre Federico Lombardi, Msemaji mkuu wa Vatican anaelezea kusikitishwa kwa Vatican kutokana na mauaji ya kinyama ya vijana watu kutoka Israeli kwamba, hivi ni vitendo ambavyo haviwezi kukubalika hata kidogo kwani ni kizingiti katika mchakato wa kutafuta amani ya kudumu, changamoto ya kuendelea kusali na kujibidisha kutafuta amani.

Vita inachochea vita na kusababisha chuki na uhasama. Baba Mtakatifu Francisko anaungana na familia za wale wanaoomboleza kutokana na mauaji ya watoto wao na anamwomba Mwenyezi Mungu mwingi wa huruma na mapendo, aweze kuwagusa watu wengi zaidi ili waoneshe moyo wa huruma na amani.









All the contents on this site are copyrighted ©.