2014-06-28 08:35:06

Askofu mkuu Jozef Wesolowski avuliwa nyadhifa zake zote!


Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa limehitimisha kusikiliza kesi na hatimaye limeamua kwamba, aliyekuwa Askofu mkuu Jozef Wesolowski, Mwakilishi wa Vatican nchini Jamhuri ya Watu wa Domenikan kutokana na kukengeuka kwake kimaadili anavuliwa dhamana zote kama Mkleri na hivyo tangu sasa hataruhusiwa kuendelea na utume wake kama Mkleri.

Adhabu hii itaanza kutekelezwa baada ya miezi miwili, wakati ambapo Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa likiendelea kusubiri rufaa kutoka kwa Jozef Wesolowski. Baada ya hukumu hii, utekelezaji wa kanuni zote zinazohusiana na ukubwa wa kosa lake zitaanza kutekelezwa!







All the contents on this site are copyrighted ©.