2014-06-25 11:48:02

Majadiliano ya kidini yanapania kujenga uelewano na urafiki


Padre Miguel Angel Ayuso Guixot, Katibu mkuu wa Baraza la Kipapa la majadiliano ya kidini pamoja na ujumbe wake kuanzia tarehe 22 hadi tarehe 27 Juni 2014 wako nchini Indonesia ili kukoleza majadiliano ya kidini, kielelezo cha kuheshimiana na ujenzi wa urafiki kati ya watu, kama anavyokazia Baba Mtakatifu Francisko. Indonesia ina waamini wengi wa dini ya Kiislam.

Padre Guixot na ujumbe wake, wanaendelea kukutana na kuzungumza na baadhi ya wajumbe wa Baraza la Maaskofu Katoliki Indonesia pamoja na taasisi ambazo zinajikita katika majadiliano ya kidini. Wanatarajia pia kukutana na kuzungumza na viongozi wakuu wa dini ya Kiislam nchini Indonesia.







All the contents on this site are copyrighted ©.