2014-06-25 16:22:41

Hakuna ukristu kwa kuwa mbali na Kanisa - Papa aonya


Jumatano hii asubuhi mahujaji na wageni zaidi ya thelathini elfu, walikusanyika katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Vatican, kusikiliza mafundisho ya Papa Francisko. Hii ilikuwa ni Katekesi ya mwisho katika muhula huu, kabla ya kuwa katika kipindi cha mapumziko ya wakati wa majira ya joto. Baba Mtakatifu aliendelea kuzamisha mafundisho yake katika mfululizo wa tafakari juu ya kanisa , hii ikiwa ni mara ya pili, katika mfululizo huo. Papa hasa alilenga juu ya Kanisa la Ulimwengu na asili yake ya kuwa la wote, na hasa juu ya umuhimu wa kuwa sehemu ya Kanisa.


Kwa kifupi katika Katekesi hii Papa ilijadili mambo matatu muhimu, muumini katika mahusiano yake na Kanisa, kama sehemu ya kanisa, akisema kwamba , haiwezekani mtu binafsi kujifungua mwenyewe tu na kujiita Mkristo, kwa kuwa Mkristo ni kuwa sehemu ya kanisa na inamaanisha kwamba ni kuungana na wana kanisa wengine, ambao kwa hiari yao wanamwungamia Yesu Kristo kuwa ndiye Bwana Mkombozi wa Ulimwengu dhidi ya dhambi na mauti. Na hivyo ni kuwa sehemu ya utamaduni hai wa Kanisa, ambalo huundwa katika Umoja wa utamaduni hai wa Imani, unaokuwa kigezo cha lazima na muhimu katika neema ya upatanisho , neema ya mnang'amuzi na uhusiano na Bwana.


Papa aliendelea kueleza kwamba, wale wanao amini kwamba, wanaweza binafsi, moja kwa moja, kujenga uhusiano wa karibu na Yesu Kristo nje ya ushirika na upatanishi wa kanisa, wanajidaganya kwa kuwa Kristu mwenyewe alianzisha usahariki huu wa Kanisa , na alipenda sana kuona wafusi wake kuwa na umoja kama yeye alivyommoja na baba yake.

Papa Francisko anasema Imani kama hii ya kujitenga na wanakanisa wengine ni jambo la hatari na kishawishi chenye madhara, kwa sababu uhusiano na Kristo licha ya kuwa jambo binafsi lakini si binafsi kwa kuwa huzaliwa na kutajirishwa na ushirika wa Kanisa.Baba Mtakatifu aliendelea kusema, hija yetu ya pamoja si rahisi. Kuna wakati tunapambana na udhaifu wa kibinadamu, mapungufu na hata kashfa katika maisha ya Kanisa.

Hata hivyo, aliendelea, Mungu ametuita kumjua na kumpenda kupitia upendo wetu kwa ndugu zetu wake kwa waume, na kudumu katika ushirika wa kanisa na kwa kutafuta katika mambo yote, kukua katika imani na utakatifu kama viungo vya mwili mmoja wa Kristo, yaani Kanisa lake.


Baada ya Katekesi kama ilivyo kawaida alisalimia katika lugha mbalimbali kulingana na makundi makubwa ya watu waliofika kumsikiliza . Kati ya kundi la wanaozungumza Kiingereza ilikuwa ni ujumbe kutoka Chuo kikuu cha Bethlehemu ambacho mwaka huu kina adhimisha miaka 40 tangu kuanzishwa kwake.










All the contents on this site are copyrighted ©.