2014-06-23 15:40:56

Papa: anayehukumu wengine ni mnafiki, na hujiweka katika nafasi ya Mungu


Baba Mtakatifu Francisko ameonya dhidi ya tabia ya kupenda kuhukumu wengine bila kutafakari hali zetu wenyewe. Kupenda kujiona sisi tu safi na yule ni mdhambi. Lakini tukumbuke kipimo kilekile tunacho tumia kuhukumu wengine, ni hichohicho kitakacho tumika kutuhukumu... Anayehukumu ndugu yake, naye atahukumiwa kwa njia hiyo hiyo. Mungu ndiye pekee "hakimu". Na mshutumiwa anaweza daima hutetewa na Yesu. Yesu, Wakili Mkuu wa Kwanza, na Wakili wa pili ni Roho Mtakatifu. Papa Francisko amesema katika hotuba yake ya wakati wa Ibada ya Misa, asubuhi Jumatatu , katika Kanisa dogo la Mtakatifu Martha, ndani ya Vatican.

Papa Francisko ameonya dhidi ya kuwa watu wa kupenda kuhukumu wengine katika nafasi mbalimbali, kimaisha,au katika uwajibikaji au mamlaka akieleza kwamba jambo kuhukumu ni hatari kwa sababu licha ya kuuumiza wengine, pia, humgeukia mwenyewe na kuishia kuwa mwathirika wa ukosefu wa huruma kwa wengine. Hiki ndicho hutokea katika kuwahukumu wengine.
Papa Francisko alitoa onyo hili, mara baada ya kusoma kifungu cha Injili kuhusu kibanzi na boriti iliyoko katika jicho, akibainisha kwamba , ni wazi inaonyesha mtu anayependa kuhukumu wenzake kuwa anafanya makosa , na huonyesha udhaifu wa mtu wa kushindwa, maana binadamu hana haki ya kumhukumu mtu mwingine kiroho, hakimu ni Mungu peke yake . Kuhukumu wengine ni "unafiki", kama Yesu alivyowaambia kwa mara kadhaa walimu wa sheria, wakati wa matukio kadhaa kwa wakati ule. Na pia ni kwa sababu Papa alieleza, binadamu hutoa hukumu yake harakaharaka, wakati hukumu ya Mungu huchukua muda.


Na hivyo , kutokana na hili , kuhukumu wengine ni makosa , kwa maneno mepesi ni kwa sababu ni kuchukua nafasi isiyokuwa yako. Na si tu ni makosa lakini pia ni kumchanganya mtu. Ni kupagawa na nia kali za kutaka kujitakatifusha, kuonekana kama safi na wengine ni wakosaji , nia zinazowasha moto wa ndani ambazo haziachi nafasi ya utulivu, wa kujitafakari wenyewe. Lakini tunaambiwa kwanza toa boriti katika jicho laki ndipo utoe kibazi kilicho ndani ya ndugu yako.

Homilia ya Papa imesisitiza , mwenye uwezo wa kutoa hukumu ni Mungu peke, na kuongeza, kile kinacho onyesha tabia ya kumtegemea Yesu,ni mfano wake wa kuto hukumu wengne.
Yesu mbele ya Baba, kamwe hakuwatuhumu wengine.Kinyume aliwatetea! Anakuwa Mtetezi wa kwanza. Kisha anampeleka mtetezi wa pili, ambaye ni Roho Mtakatifu. . Yeye ni Wakili mbele ya Baba dhidi ya mashtaka, Papa ameeleza na kuhoji Na ni nani basi mshitaki? Na kutoa jibu la Biblia,kwamba Mshitaki anaitwa Ibilisi , shetani. Na hivyo Mwisho wa Dunia, Yesu atahukumu lakini wakati huo huo ni mwombezi na mtetezi ..

Hatimaye, Papa Francisko , alisema, anayehukumu, humwinga Mkuu wa ulimwengu huu,ibilisi ambaye daima ni nyuma ya watu, akitaka kuwashtaki kwa Baba. Lakini Bwana, atatupa neema ya kumwiga Yesu, wakili na mwanasheria wetu. Na si kuwaiga wengine, ambayo mwisho wao ni huangamiza

Papa ameasa, iwapo tunataka kutembea katika njia ya Yesu, tunapaswa kuwa mawakali watetezi wale wanaotuhumiwa mbele ya Baba. Kwa namna gani tunaweza kuwa watetezi wa wengine wanaoshutumiwa, je ni kuingilia kati mara ? Hapana ni kukaa kimya na kwenda kusali na kumtetea mbele ya Bwana kama Yesu alivyofanya msalabani. Kusali kwa ajili yake na si kuhukumu. Ni vibaya kuhukumu kwa sababu, pia utahukumiwa

Papa aliwataka wote waliokuwa wakimsikiliza kukumbuka hilo siku zote , pale inapokuja hamu ya kutaka kuhukumu wengine , na kusema mabaya ya wengine, kuyashihnda majaribu hayo kwa kusali na kuomba neema ya kusamehe wengine..








All the contents on this site are copyrighted ©.