2014-06-19 10:34:42

Usikate tamaa!


Waamini wanaweza kuonja uwepo endelevu wa Yesu Kristo katika hija ya maisha yao ya kiimani kwa njia ya Neno la Mungu; Sakramenti za Kanisa, lakini kwa namna ya pekee Sakramenti ya Ekaristi Takatifu, kumbu kumbu endelevu ya mateso, kifo na ufufuko wa Yesu.

Kwa njia ya Fumbo la Ekaristi Takatifu, Yesu anajisadaka tena Altareni ili aweze kuwa ni chakula na kinywaji cha maisha ya kiroho! Yesu anajionesha pia katika matukio ya kila siku, lakini zaidi miongoni mwa maskini na wote wanaosukumizwa pembezoni mwa Jamii! Hapa unaweza kuonja uwepo endelevu wa Yesu!

Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii anasema kwamba, hakuna sababu msingi ya mwamini kutokuwa na matumaini, kwani Yesu amewahakikishia kwamba, atakuwa pamoja nao hadi utimilifu wa dahali!







All the contents on this site are copyrighted ©.