2014-06-13 15:11:57

Papa Francisko kuhudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Lishe.


(FAO) Mkurugenzi Mkuu José Graziano da Silva, wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) Jumatano katika mkutano na waandishi , alieleza kwamba, Papa Francisko , ameridhia kuhudhuria Mkutano wa pili wa Kimataifa juu ya lishe, ambao utafanyika katika Makao Makuu ya FAO Roma, hapo tarehe Novemba 19-21 2014. Papa atajiunga katika mkutano huo,Novemba 20.

Mkutano wa pili wa lishe unafanyika baada ya kupita miaka 22 ya kuwa na mkutano kama huo, kama inavyoandaliwa kwa ushirikiano wa FAO na WHO. Kwa mujibu wa FAO, katika miongo hiyo miwili, maendeleo katika hatua za kupunguza njaa na utapiamlo , zimefanyika taratibu sana katika kiwango kisicho kubalika. Makadirio ya FAO yanaonyesha kwamba, mwaka 2011-2013 kulikuwa na watu zaidi ya millioni 842,000,000 ambao hawakuwa na lishe ya kutosha, Na karibia asilimia 45% ya watoto milioni wapatao 6.9 walikufa kwa ukosefu wa lishe bora, ambamo pia kati yao watoto 99,000,000 wana uzito pungufu
.

Askofu Mkuu Luigi Travaglino, Mtazamaji wa Kudumu wa Jimbo la Papa katika Shirika la Chakula na Kilimo , FAO, akijibu swali la waandishi wa habari , umuhimu wa Papa katika mkutano wa lishe wa Novemba na wajibu wa Kanisa katika kupambana na njaa , kwanza alionyesha kushangazwa na maswali hayo yanayoonyesha kutotambua historia ya utume wa Kanisa katika jamii.

Askofu Travaglino alisema kuhusu mwaliko wa Papa, mwanzo wa uwepo wa Makao Makuu ya FAO hapa Rome, Baba Mtakatifu daima amekuwa miongoni mwa wajumbe wa kwanza kualika katika mikutano mikuu ya FAO, kama jambo la kawaida la kimaadili, kutokana na malengo yake ya , kuwatumikia wengine, na kuwasaidia wengine. Kanisa hujadili juu ya mwingine, jirani. FAO, kama taasisi ya walei, huzungumzia kuhusu binadamu kama ilivyo kwa Kanisa.

Na wa swali la pili, Kanisa hufanya nini kupambana na njaa, utapiamlo, anasema, alisema pia jibu la hili liko katika uzoefu na shuhuda kwa wale wenye macho ya kuona kwa sababu hakuna nchi hata moja duniani, ambako Mama Kanisa hajali hali za watu. Askofu Mkuu Travaglino, alieleza kwa kutoa uzoefu wake katika nchi alizotembelea au kufanya kazi , Afrika na Amerika ya Kusini, ambako Kanisa linajitahidi kwa njia mbalimbali kusaidia watu masikini kupambana na njaa na umaskini. Na karibu uwakilishi wote wa Kanisa , , au Mkristo, au muumini; ujitahidi kuendelea kutoa mchango, kama sehemu ya utume wa kanisa katika kumpenda jirani na kwa ajili ya kudumisha heshima ya mwanadamu.

Na Mkurugenzi Mkuu José Graziano da Silva, akijibu swali juu ya mahusiano kati ya FAO na Jimbo la Papa amesema, tangu nyakati za mwanzo wa FAO, kumekuwa na mahusiano mazuri ya karibu na Baba Mtakatifu. Na si tu katika joto la kijuujuu lakini hasa katika uhusiano wa kupanga pamoja mipango adilifu na usawa kimaadili katika mapambano dhidi ya ubaguzi wa kijamii, umaskini na njaa, ambavyo daima zimekuwa katika ajenda ya Kanisa Katoliki na pia katika ile ya FAO. Kwa pamoja hufanya kazi ya kichungaji ya Kanisa, kwa mfano, katika Brazil husaidia kuwaongoza watu , kwa ajili ya kuwafanikisha kulisha familia zao ambazo zina idadi kubwa ya watoto, ili kuweza pia kuwa na mali zisizo hamishika. Na pia kuwa na mipango shirikishi ili watoto wasikose mahitaji ya chakula bora, ili wasipungukiwe na madini mwilini , hasa matunda na mboga.

José Graziano da Silva, aliendelea kujibu swali juu ya watakazozungumza watakapokutana na Papa Francisko, akisema, kwa wakai huu ni vigumu kusema chochote juu ya uwepo wa Papa Francisko katika mkutano wa Novemba, isipokuwa kutoa shukurani kwake Papa . Ni kutoa asante kwa msaada wake kwa ajili ya kazi ya FAO. Naamini uwepo wa Papa Francisko mbele yao utaweza kuwahamasisha wote si tu kufanya zaidi, lakini katika hisi za aina ya ushirikiano uliopo kwamba, si tu Kanisa Katoliki, lakini dini zote, juu ya suala la uhakika wa chakula na mapambano dhidi ya njaa.

Da SIlva, aliendelea kutaja uzoefu wake aliopata Brazil kwamba, unamruhusu kusema kwamba, utendaji wa makanisa kwa ujumla, huwa jukumu muhimu sana, kwa sababu, katika hali nyingi, huwafikia watu maskini, wenye njaa, hata wale wasioonekana. Watu ambao hawajulikani wanakoishi na hata serikali haina takwimu zao. Watu hawa hawako katika mipango ya misaada ya kiserikali, Lakini Kanisa ilinatambua waliko na huwa na mipango ya kutoa msaada kwa watu hao.








All the contents on this site are copyrighted ©.