Wamissionari wa Shirika la Damu Azizi ya Yesu, Vikarieti ya Tanzania wamehitimisha
mkutano mkuu wa uchaguzi uliokuwa unafanyika Jimboni Dodoma na kusimamiwa na Padre
Oliviero Magnone, mkuu wa Shirika la Wamissionari wa Damu Azizi ya Yesu Kanda ya Italia.
Majembe yaliyochaguliwa kuliongoza Shirika katika kipindi hiki cha mpito kwa Tanzania
kuwa Jimbo kamili linalojitegemea ifikapo mwaka 2015.
Waliochaguliwa kwenye
mkutano mkuu wa tano wa Shirika la Wamissionari wa Damu Azizi ya Yesu Vikarieti ya
Tanzania ni:
Padre Reginald Mrosso, C.PP.S. Mkuu wa Shirika. Padre Gregory
Mkhotya, C.PP.S. Makamu mkuu wa Shirika. Padre Egidius Seneda, C.PP. S. Katibu
mkuu. Padre Francis Bartoloni, C.PP.S. Mshauri. Padre Richard Kungi, C.PP.S.
Mtunza fedha.