Papa apendekeza mashindano ya kombe la Dunia iwe ni Siku Kuu ya amani duniani
Baba Mtakatifu Francisko, amepeleka ujumbe wa matashi mema kwa njia ya video kwa
washiriki wote wa michezo ya mashindano ya kombe la Dunia la Mpira wa miguu, yanayotazamiwa
kuanza hivi karibuni, Brazil. Amesema, "napenda kutuma salamu zangu za dhati kwa
waandaaji, wafanikishaji na kwa kila mwanamichezo na mashabiki, pia kwa watazamaji
wote wa njia ya televisheni, radio na internet, na washiriki wote wa tukio hili linalovuka
mipaka yote ya lugha, utamaduni na kitaifa. Katika ukweli, mpira wa miguu una tunu
nyingi katika mahusiano ya binadamu hivyo si mashindano tu lakini pia huwa na manufaa
katika mitazamo mingine ya kimaisha , na hasa katika ujenzi wa haki na amani. Michezo
ni shule ya amani , hufundisha uvumilivu katika kujenga amani".
Papa ameonyesha
matumaini yake kwamba, pamoja na maadhimisho ya michezo ya Kombe la mpira wa miguu
la Dunia, pia madhumuni yake yanaweza kubadilishwa na kuwekwa kama ni Siku Kuu ya
Mshikamano kati ya watu. Katika ujumbe huu, Papa anasema Michezo si tu wakati
wa kujifurahisha , lakini pia ni huonyesha jinsi binadamu anavyoweza kushirikiana
katika kukuza tunu msingi za katika utu wa mtu, na ujenzi wa amani na maelewano na
umoja . Na hivyo mashindano ya mpira wa miguu licha ya kuwa tu aina ya burudani, lakini
pia alisisitiza Papa, inakuwa ni nyenzo ya kuonyesha uadilifu ambamo utu na uzuri
wa binadamu hukuzwa na kusaidia kujenga amani zaidi na mshikamano na udugu. Katika
michezo, tunaona kwamba inawezekana kuishi kwa uaminifu, uvumilivu, urafiki, kugawana,
kushirikishana na mshikamano. Kwa kweli, mpira wa miguu hufufua uadilifu kwa wengi
na si tu wakati wa mashindano ya mpira kwenye uwanja wa mpira , lakini pia katika
nyanja zote za maisha, hasa zaidi katika ujenzi wa amani. Papa anaendelea kusema,
michezo ni shule ya amani, inatufundisha kujenga amani, kupitia kujifunza kutunza
uaminifu haki na kuheshimiana, kati ya wapinzani. Michezo hutufundisha kwamba , ni
lazima kufanya bidii katika kupata mafanikio ya kuwa mshindi . Kwa namna hiyo, tunaweza
kuona mchezo huu wa mpira wa miguu, kama mfano katika utendaji wa maisha yetu. Katika
maisha ni muhimu kupambana, kujitahidi kupata matokeo mazuri. Kiroho, michezo hutukumbusha,
mfano wa kuongeza bidii katika majitoleo kama sadaka muhimu ya kukua katika fadhila
na majiundo ya tabia ya mtu. Ni lazima kuwa na mafunzo makali kwa ajili ya kumboresha
mtu katika uchezaji wake na hivyo ndivyo anavyokua katika ahadi zake za kuwa mwaminifu
, adilifu na mtu wa haki na amani kati kati ya watu na watu wema!
Mpira wa
miguu, unaweza na inapaswa kuwa shule kwa ajili ya majiundo ya kujenga utamaduni
wa kukutana, wenye kuleta maelewano na amani miongoni mwa watu. Na hapa tunapata
somo la pili juu ya mchezo, kwmba ni kucheza kwa haki. Kucheza kama timu kunahitaji
ufahamu zaidi ya yote ni kwamba , kwanza ni kwa ajili ya manufaa ya timu zima, na
si kwa manufaa binafsi. Katika kupata ushindi ni lazima kuushinda ubinafsi, ubinafsi
katika kila hali na kila aina ya ubaguzi, iwe kikabila, kimbali , rangi, utaifa n.k
. Badala yake ni uvumilivu na kutunza utu wa mtu, kwa kuwa ubinafsi katika mpira
wa miguu ni kikwazo kwa mafanikio ya timu; na ndivyo ilivyo , kama tunakuwa na ubinafsi
katika maisha, kwa kuwapuuza watu walio karibu nasi, tunaumiza jamii nzima.
Papa
aliendelea kutaja somo la mwisho la michezo ya kufikia amani, ni heshima sahihi kati
ya wapinzani. Alieleza siri ya ushindi, iwe uwanjani au katika maisha, iko katika
kujua jinsi ya kumheshimu mchezaji mwingine, hata kama ni mpinzani wetu. Hakuna
mafanikio katika ubinafsi, iwe uwanjani, au katika maisha! Na kwamba, wanaojitenga
hujisikia kutengwa! Na, kama ulivyo ukweli kwamba, mwishoni mwa mashindano, timu
moja hupata ushindi , kama ilivyo katika mashindano haya ya Kombe la Mpira wa miguu
la Dunia, ni timu ya taifa moja tu itakayoinua kikombe juu kama mshindi. Lakini katika
ukweli, washiriki wote wa mashindano haya ni washindi katika kuwa adilifu, na katika
kudumisha haki na umoja. wote ni washindi katika uimarishaji wa uimarishaji wa viungo
vya umoja na mshikamano wa binadamu.
Papa alimalizia hotuba yake, kwa kumshukuru
Rais wa Brazil, Bi Dilma Rousseff, kwa salaam zake, na alimhakikishia kwamba anatolea
sala zake kwa Mungu ili mashindano haya ya Kombe la Dunia yafanyike kwa kila utulivu,
kuheshimiana, mshikamano na udugu kati ya wake kwa waume, wakijitambua kama ni watu
wa familia moja. Asante.