2014-06-12 10:47:28

Bara la Afrika linaendelea kucharuka kiuchumi! Lakini Pochi hakuna!


Licha ya majanga mbali mbali yanayoendelea kujitokeza nchini Nigeria, lakini bado Nigeria inaendelea kucharuka katika masuala ya kiuchumi na kwamba, inaonekana kuwa na mvuto mkubwa kwa wawekezaji kutoka Barani Ulaya na Marekani. Utafiti uliofanywa na Jarida la kiuchumi lijulikanalo kama Wall Street Journal, kuhusu mwenendo wa soko katika masuala ya uchumi. Kati ya nchi 20 zinazoendelea kuibukia katika masuala ya kiuchumi, kuna nchi 11 kutoka Barani Afrika.

Takwimu hizi zinaonesha kwamba nchi zinazoongoza kutoka Afrika ni kama ifuatavyo:
1. Nigeria ni nchi ya kwanza kwa kuwa na asilimia 29.5%.
2. Kenya inayochukua nafasi ya tano kwa kuwa na asilimia 23.17%.
3. Angola inachukua nafasi ya sita kwa kuwa na asilimia 21.9%.
4. Ghana inachukua nafasi ya tisa kwa kuwa na asilimia 18. 73%.
5. Ethiopia inachukua nafasi ya 11 ikiwa na asilimia 17. 27%.
7. Morocco inashikilia nafasi ya 12 ikiwa na asilimia 16.79.
8. Tanzania inashikilia nafasi ya 13 kwa kuwa na asilimia 16.79.
9. Algeria inashikilia nafasi ya 14 kwa kuwa na asilimia 16.06%.
10. Pwani ya Pembe inashikilia nafasi ya 16 kwa kuwa na asilimia 14.58.
11. Zambia inashikilia nafasi ya 17 kwa kuwa na asilimia 13.63%.
12. Uganda inashikilia nafasi ya 19 kwa kuwa na asilimia 13.14.

Taarifa hii inaonesha mwelekeo wa uwekezaji kutoka katika makampuni ya kimataifa yanayotaka kuwekeza Barani Afrika. Kiashilia kinaonesha ni asilimia kiasi gani wawekezaji kutoka nje wamevutiwa na nchini husika. Ikiwa kama idadi ya Makampuni ya Kimataifa 50 kati ya 200 yanaonesha kuvutiwa na nchi husika, nafasi yake ni 25%. Makampuni makubwa ya kimataifa yanaendelea kuonesha nia ya kuwekeza Barani Afrika ili kushiriki katika mchakato wa maendeleo ya watu wa Bara la Afrika.

Mradi wa umeme Barani Afrika uliotangazwa na Serikali ya Marekani utanufaisha watu millioni 240 kutoka Barani Afrika katika nchi za: Ethiopia, Ghana, Kenya, Nigeria, Liberia na Tanzania. Mwezi Agosti kunatarajiwa kufanyika kwa Jukwaa la Maendeleo kati ya Bara la Afrika ya Singapore, ili kuimarisha ushirikiano katika masuala ya biashara kati ya Afrika ya Nchi kutoka Asia.







All the contents on this site are copyrighted ©.