2014-06-10 11:11:06

Tanzia: Kardinali Bernard Agre amefariki dunia.


Tunasikitika kutangaza kifo cha Kardinali Bernard Agre, kilichotokea Tarehe 9 Juni 2014, Jumatatu asubuhi. Marehemu Kardinali Agre alikuwa ni Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu la Abidjan (Ivory Coast). Amefariki akiwa na umri wa miaka 88, akiwa hospitalini Paris,ambako alikwenda kupata matibabu.
Kwa kifo chake, Chuo cha Makardinali kwa sasa kimebaki na Makardinali 213 ambao kati yao 118 ni wapiga kura na 95 hawana haki ya kupiga au kupigiwa kura katika kikao cha kumchagua Papa, kwa mujibu wa sheria ya umri iliyopo.

Wasifu:Kwa kifupi, Kardinali Bernard Agre , alizaliwa Monga , Machi 2, 1926, Jimbo Kuu la Abidjan na Baba Jean Manda na Jeanne Yomin. Alibatizwa Septemba 2, 1932 katika Parokia ya Memni.
Alipata elimu yake ya msingi katika shule ya Mission Katoliki ya Memni 1936-1941.
Kutoka 1941-1947 alihitimu masomo ya sekondari katika seminari Ndogo ya Bingerville. Alianza masomo ya falsafa katika Seminari Kuu ya Bingerville (1947-1948). Na alikubaliwa kujiunga na Seminari Kuu ya Quidah, ya Dahomey (sasa Benin), 1948-1953 na kukamilisha masomo yake ya kiteolojia.
Alipadirishwa Julai 20, 1953 katika Seminari ndogo ya Bingerville.
Baada ya utumishi mbalimbali katika Jimbo lake , mwaka 1957, alijiunga na masomo katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana Roma, ambako aliipatia shahada ya uzamili mwaka 1960, katika teolojia, na sheria za Kanisa.
Alirudi Ivory Coast, na kwa miaka miwili baada ya kuwa Paroko wa Parokia ya Notre Dame Treichville,na alifanywa kuwa Vika Mkuu wa Jimbo Kuu la Abidjan.

Aliteuliwa kuwa Askofu wa Man Abidjan , Juni 8, 1968, na kuwekwa wakfu Oktoba 3 ya mwaka huohuo, utume alioutumikia hadi Machi 25, 1992 alipoteuliwa kuwa Askofu wa Jimbo jipya la Yamoussoukro, ambalo alianza kuliongoza rasmi Mei 17, 1992. Miaka miwili na nusu baadaye, Desemba 19, 1994 aliteuliwa Askofu Mkuu wa Abidjan. Alichukua milki ya Jimbo kuu hilo Februari 26, 1995.

Katika ngazi ya kimataifa, 1972-1996, alishika nafasi ya Mwenyekiti wa Tume ya Maaskofu kwa ajili ya Mawasiliano Jamii, katika Baraza linalounganisha Mabaraza ya Maaskofu ya Mkoa Maaskofu wa Afrika Magharibi (CERAO).
Kutoka 1985-1991 alikuwa Rais wa CERAO.Mwaka 1993 aliteuliwa Rais wa Kamati ya Maaskofu Pan-African kwa ajili ya Mawasiliano Jamii (CEPACS), Na pia alikuwa Mjumbe katika Kamati ya kwa sherehe ya Jubilei Kuu ya Mwaka 2000.
Na Rais wa Mkutano Mkuu Sinodi ya Kawaida wa 10 Maaskofu (Oktoba 2001).
Tangu 2 Mei 2006, alistaafu kuwa Askofu Mkuu Mstaafu wa Abidjan.

Papa John Paul II alimteua kuwa Kardinali katika kikao cha Consistory cha a 21 Februari 2001, na kuwa Askofu Mkuu wa jina wa Kanisa la Mtakatifu Yohana Chrysostom lililoko Monte Sacro Altovyeo alivyobaki navyo hadi kifo chake. Tunamwombea Bwana ampokeee katika mikono yake ya uzima wa milele.








All the contents on this site are copyrighted ©.