Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe amtembelea Papa mjini Vatican
Baba Mtakatifu Francisko Ijumaa tarehe 6 Juni 2014 amekutana na kuzungumza na Bwana
Lech Walesa na ujumbe wake kutoka Poland. Viongozi hawa wameshirikishana masuala mbali
mbali ya kimataifa na kitaifa. Baba Mtakatifu pia amekutana na kuzungumza na Waziri
mkuu wa Japan Bwana Shinzo Abe pamoja na ujumbe wake mjini Vatican ambao wamejadili
masuala ya msingi katika medani za kimataifa. Waziri mkuu wa Japan amelishukuru Kanisa
kwa msaada wake wa hali na mali wakati Japan ilipokumbwa na Tsunami
Waziri
mkuu wa Japan amemzawadia Baba Mtakatifu Francisko kioo cha muujiza kilichokuwa kinatumiwa
na Wakristo wakati wa madhulumu ili kuonesha Msalaba na Sura ya Yesu kinapokutana
na Mwanga. Amemzawadi pia Picha ya Balozi wa kwanza wa Japan aliyefika mjini Vatican
kunako mwaka 1615 ili kuomba msaada wa Wamissionari kutoka katika Kanisa Katoliki,
ili kusaidia mchakato wa Uinjilishaji nchini Japan na Picha ya Pili inamwonesha Mtumishi
wa Mungu Papa Paulo VI, ambaye Waziri mkuu aliwahi kukutana naye katika maisha yake!
Baba
Mtakatifu Pia amepatia mgeni wake zawadi ya medali ya Mtakatifu Petro alipokuwa anaokolewa
kutoka Gerezani kama inavyooneshwa kwenye Kitabu cha Matendo ya Mitume 12: 1-17.
Waziri
mkuu wa Japan Bwana Shinzo Abe amekutana na kuzungumza pia na Kardinali Pietro Parolin,
Katibu mkuu wa Vatican pamoja na ujumbe wake.