2014-06-02 09:11:22

Jiwekeni tayari kuhudumia!


Katika Maadhimisho ya Siku kuu ya Bikira Maria kumtembelea Elizabeth, ambayo inaadhimishwa kila mwaka ifikapo tarehe 31 Mei, Baba Mtakatifu Francisko ametumia fursa hii kufunga rasmi mwezi uliotengwa na Mama Kanisa kwa ajili ya Ibada kwa Bikira Maria kwa kushiriki kusali Rozari na waamini waliokuwa wamekusanyika kwenye Bustani za Vatican.

Baba Mtakatifu anasema, baada ya Bikira Maria kupashwa habari na Malaika kwamba atakuwa ni Mama wa Mungu kwa njia ya Roho Mtakatifu na habari kuhusu binamu yake Elizabeth kupata ujauzito, aliondoka haraka kwenda kumhudumia. Ni Mama ambaye yuko tayari kuwasikiliza na kuwasaidia wale wote wanaokimbilia ulinzi na tunza yake ya kimama. Bikira Maria ni mama asiyepoteza wakati yuko tayari kuhudumia!







All the contents on this site are copyrighted ©.