2014-05-31 10:32:54

Papa atoa daraja la Uaskofu kwa katibu mpya msaidizi wa Sinodi za Maaskofu


(Vatican Radio) Papa Francisko, siku ya Ijumaa jioni aliongoza Ibada ya misa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, kwa nia ya kutoa daraja la Uaskofu kwa Padre Fabio Fabene, aliyemteua kuwa Katibu Mkuu Msaidizi , katika secretariati ya wa Sinodi za Maaskofu Vatican.
Homilia ya Papa , ikilenga zaidi katika liturujia ya utoaji wa daraja la Uaskofu, ilielekea zaidi katika wito huu muhimu wa utume wa ofisi ya askofu, na jukumu na wajibu wake mkubwa katika kujenga uhusiano kwa wote, Mungu na Waamini. Na kwamba, Askofu kwa kweli,ni huduma, na si heshima, kwa vile kufanywa Askofu ni kuitwa katika utumishi zaidi, na si kutawala.

Askofu Fabene , alizaliwa mwaka 1959 na alipadrishwa kama Padre wa Jimbo la Viterbo, mwaka 1984 na aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu Msaidizi katika Ofisi ya Sectretariat ya Vatican kwa ajili ya Sinodi, Aprili 8 mwaka 2014.

Baba Mtakatifu alisema, Bwana wetu Yesu Kristo , alitumwa na Baba kuwakomboa watu, nae aliwatuma mitume wake duniani kote , wakiwa wamejawa na nguvu za Roho Mtakatifu, waliitangaza injili kwa mataifa yote, na kuwaleta pamoja chini ya mchungaji mmoja , na kuwatakasa na kuwaongoza katika wokovu.

Ili kuendeleza kizazi hadi kizazi huduma hii ya kitume, Mitume kumi na wawili, wakusanyika pamoja na wasaidizi wao walio wawekea mikono, zawadi ya Roho Mtakatifu, walio mpokea kutoka kwa Kristo , ambaye ni ukamilifu wa sakramenti ya Daraja takatifu . Hivyo , hatua hiyo inaendelezwa kwa mfululizo na Maaskofu katika utamaduni wa maisha ya Kanisa wenye kuilinda huduma hii msingi na kazi ya Mwokozi inaendelea na kukua hadi nyakati zetu.

Askofu huzungukwa na Mapadre wake, yeye akiwa katikati sawa na Bwana wetu Yesu Kristo , Padre Mkuu wa milele. Ni Ukweli kwambaKristo katika huduma ya Askofu, huendelea kuhubiri injili ya wokovu na utakaso wa waumini kwa njia ya sakramenti.Ni Kristo kupitia huduma ya Askofu huongeza waumini wapya katika Mwili wake ambao ni Kanisa. Askofu kwa hekima na busara anazochota kutoka kwa Kristo, huwaongoza watu wa Mungu katika Hija ya maisha ya kidunia na furaha ya milele .

Papa Francisko alieleza na kusema, hivyo wana furaha kuu ya kumpokea mteuliwa mpya Askofu Fabene katika kundi la Maaskofu, na kwa kumwekea mikono, sasa anajiunga na Chuo cha Maaskofu. Ni kumpa heshima ya kuwa mtumishi wa Kristo na wakili wa siri za Mungu , ambayo ni dhamana na ushuhuda wa injili na huduma ya Roho ajili ya utakatifu. Papa pia alikumbusha maneno ya Yesu na Mitume : "awasikilizae ninyi anaisikiliza mimi naye awakataaye ninyi anikataa mimi , naye anikataaye mimi, amkataa yeye aliyenituma "(Luka 10:16).

Na alimkumbusha Askofu mpya kuwa mfumo wa uongozi wa Kanisa, inayowaunganisha viongozi wote wa Kanisa pamoja kwa kifungo cha upendo , ndivyo anavyopaswa kubeba ndani ya moyo wake, umoja na mshikamano huo wa kanisa , kwa ukarimu wa kuokoa wale hasa wanaohitaji zaidi msaada. Na alionyesha imani yake kwamba, hili litakuwa rahisi kwake, kupitia kazi aliyokabidhiwa katika Sekretarieti ya Sinodi ya Maaskofu.

Papa pia alitoa wito wa kukesha macho, kwa ajili ya kulilea kundi lote kwa upendo , ambamo Roho Mtakatifu huliongoza Kanisa katika kulitawala Kanisa la Mungu . Aliongeza ni kukesha macho bila kusinzia, na bila ya kuwa na hofu , kwani, kwa imani, Roho Mtakatifu atamwongoza , na kumsindikiza katika lindo hili, analo kabidhiwa rasmi katika ibada hiyo, katika jina la Roho Mtakatifu , ambaye anatoa maisha kwa Kanisa na kwa uwezo wake, huwadumisha Maaskofu licha ya udhaifu wao wa kibindamu.








All the contents on this site are copyrighted ©.