Mshereheshaji mkuu wa Ibada za Kipapa, Monsinyo Guido Marini , kwa agizo la Baba
Mtakatifu Francisko anatangaza kwamba Alhamisi Juni 12, 2014 , saa 10 asubuhi, katika
ukumbi wa Mkutano wa Makadinali ulioko katika jengo la Kitume la Vatican, wakati
wa maadhimisho ya Masifu ya adhuhuri , kutafanyika Mkutano wa kawaida, wa Makardinali
kwa lengo la mchakato wa kutajwa Wenye Heri wafuatao katika daraja la Watakatifu,
- Giovanni Antonio Farina , askofu wa Vicenza, mwanzilishi wa Shirika la Masista
wa Mtakatifu DOROTEA Mabinti wa Mioyo Mitakatifu; - Chavara Kuriakose Elias la
Familia Takatifu , Padre na mwanzilishi wa Usharika wa Carmelites wa Maria asiyekuwa
na ndoa ; - Ludovico da Casoria , Padre wa Shirika la shirika la Ndugu Wadogo
, mwanzilishi wa Usharika wa Masista wa Elizabeti Wafransiskani; - Nicholas Longobardi
, wa Shirika la Wamini; - Eluvathingal Euphrasia ya Moyo Mtakatifu , wa Usharika
wa Masista wa Mama wa Karmeli ; - Amato Ronconi , Mwanashirika wa Kanuni ya atu
katika Shirika la Mtakatifu Francis na mwanzilishi wa Hospitali ya Wakimbizi maskini
katika eneo la Saludecio, ambako kwa sasa ni nyumba ya mapumziko ya Mwenye Heri Pia
Beato Amato Ronconi ."
Makardinali Wakazi wa Rome, siku hiyo wanaombwa kukutana
saa 9.30 katika Ukumbi wa Makaridinali ulioko mjini Vatican, wakiwa wamevaa vazi
lao rasmi.