2014-05-30 12:30:33

Toeni ushuhuda wa uaminifu katika maeneo ya kazi!


Mama Kanisa anafundisha kwamba, utu wa mwanadamu ndicho kipimo cha heshima ya kazi. Kazi ya mwanadamu ina pia asili yake kimaumbile katika upande wa kijamii. Kwa kweli kazi ya mtu mmoja imeunganika kiasili na kazi za watu wengine.

Kauli mbiu inayopaswa kuongoza mahusiano ya kazi ni "fanya kazi pamoja na wengine na fanya kazi kwa ajili ya wengine". Matunda ya kazi yanatoa fursa kwa ajili ya kubadilishana mawazo, kujenga mahusiano na vilevile kwa ajili ya kukutana bila kutegemea. Kazi ni ni haki ya msingi na ni jambo zuri kwa mwanadamu, kazi inamsaidia na kumpa thamani mtu kwa ndiyo njia ya kumwelezea mwanadamu na kumpa utu.

Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii anasema kwamba, kila Mkristo, katika eneo lake la kazi, anaweza kutoa ushuhuda kwa maneno, lakini zaidi kwa njia ya maisha yake yanayojikita katika uaminifu.







All the contents on this site are copyrighted ©.