Marais wa Israeli na Palestina kusali na Papa tarehe 8 Juni 2014
Wito wa Baba Mtakatifu Francisko kwa Marais Shimon Peres wa Israeli na Mahmoud Abbas
wa Palestina kusali kwa pamoja kwa ajili ya kuombea amani Nchi Takatifu umepokelewa
kwa mikono miwili na wahusika.
Taarifa kutoka Vatican zinaonesha kwamba, Jumapili,
tarehe 8 Juni 2014 majira ya jioni viongozi hawa wawili watakutana na kusali pamoja
na Baba Mtakatifu Francisko mjini Vatican. Hii itakuwa ni Siku kuu ya Pentekoste,
Roho Mtakatifu alipowashukia mitume! Tarehe hii imekubaliwa na Marais wote wawili.