Maaskofu wa Afrika Kusini watoa msaada kwa jumuiya inayoteseka machimboni
(Vatican Radio) Baraza la Maaskofu la Afrika Kusini, limetoa kiasi cha Rand 75,000,
kwa jimbo la Rustenburg Afrika Kusini kusaidia maelfu ya watu wanaoishi katika mazingira
magumu na walioathirika na mgomo katika machimbo ya platinum.
Migomo, huu
ulioingia katika wiki 18, ni muda mrefu zaidi na wenye vurugu zaidi katika historia
ya migodi ya Afrika Kusini. Mgodi huo wa platinum unamilikiwa na Kampuni ya Anglo
American Platinum, Impala Platinum na Lonmin inayopambana na upinzani kutoka Chama
cha Muungano wa wafanya kazi na wajenzi machimboni.
mgomo huu , unazidi
kusukuma shimoni uchumi wa taifa, na pia ghasia dhidi ya wale wasiotaka kugoma tangu
mwanzo na kusababisha watu kadha kupoteza maisha na una shamirisha hali mbaya ya
kibinadamu katika jamii ya madini na katika makazi ya jirani ambapo watu , wengi
wao wakiwa ni walioathirika na virusi vya ukimwi, na pia wanakufa kwa uhaba wa chakula
.
Askofu Kevin Dowling wajimbo la Rustenburg, Kevin Dowling , ambaye anaendesha
hospitali kubwa ya ( Tapologo ), vituo vya huduma , jikoni supu , kliniki na vituo
vya kurefusha maisha, anajitahidi kusaidia wachimba madini hao na jamii iliyo kata
tamaa Rustenburg.
Akizungumza na Linda Bordoni wa Radio Vatican alisema,
serikali kupitia waziri wake mpya kwa ajili ya madini, imeahidi kuingilia kati mazungumzo
kati ya Muungano wa wafanyakazi katika migodi na wamiliki wa migodi hiyo .