2014-05-29 10:17:15

Wito kwa Boko Haramu: Fuateni njia ya mazungumzo, upendo na kuepuka chuki.


Askofu Mkuu Mstaafu wa Douala , Kardinali Tumi Wiyghan , ametoa wito kwa Boko Haramu, kuwaachie huru bila masharti, Mapadre wawili wamisionari, wa Shirika la Italia la Fidei Donum wa jimbo la Vicenza, Padre Giampaolo Gian na Padre Antonio Allegri , pamoja na Sista Martha, Mkanada, waliotekwa nyara katika eneo la Kaskazini mwa Nigeria kati ya 4 na Aprili 5 katika Jimbo la Maroua - Mokolo kaskazini mwa Cameroon.
Kardinali Tumi ametoa wito huo kwavyombo vya habari na kupitia Shirika la habari la FIDES, ambamo amewaomba mashabiki wa kikundi cha boko haramu kuwachia wamisionari hayo bila masharti. Kardinali amesisitiza na kulaani akisema kwamba ghasia haiwezi kutatua kitu chochote, bali mamlaka ya Boko Haram, ikubali kufuata njia ya mazungumzo, upendo na kuepuka chuki kwani kuna faida zaidi.







All the contents on this site are copyrighted ©.