2014-05-29 08:51:16

Ulinzi na usalama unaendelea kuimarishwa Uganda


Wakati huu waamini wengi kutoka ndani na nje ya Uganda wanapoelekea Namgongo kwa ajili ya maadhimisho ya Siku kuu ya Mashahidi wa Uganda inayofanyika kila mwaka ifikapo tarehe 3 Juni, Vikosi vya ulinzi na usalama nchini Uganda vinaendelea kujiimarishwa ili kukabiliana na uwezekano wa mashambulizi ya kigaidi nchini humo kama inavyotokea kwa nchi jirani ya Kenya.

Ubalozi wa Marekani nchini Uganda umetoa onyo hilo na kusema kwamba, Marekani inasikitishwa na vitendo vya kigaidi vinavyoendelea kujitokeza nchini Kenya kiasi cha kuwajengea watu hofu na mashaka kuhusu usalama wa maisha na mali zao.







All the contents on this site are copyrighted ©.