Cor Unum Mwenyeji wa Mkutano wa Mashirika ya Katoliki ya Hisani Syria
Vatican Radio) Siku ya Ijumaa, Mei 30, Baraza la Kipapa " Cor Unum " litakuwa mwenyeji
wa mkutano wa uratibu wa Mashirika Katoliki ya Hisani , yanayo fanya kazi katika mazingira
ya mgogoro wa kisiasa Siria.
Mkutano huo, unajumuisha mashirika 25 yanayo fanya
kazi Syria na Mashariki ya Kati, unafanyika katika muundo wa awamu mbili, Wakati
wa asubuhi , baada ya kuwasilishwa na Kardinali Robert Sarah , Rais wa Cor Unum ,
ambaye ndiye mratibu mkuu wa kazi za Mkutano huo, kutafuatia taarifa kutoka kwa Katibu
wa Nchi wa Vatican , Kardinali Pietro Parolin .
Wasemaji ni pamoja na Askofu
Mkuu Mario Zenari , Mjumbe wa Kitume wa Papa nchini Syria, na Askofu Antoine Audo
, Rais wa Caritas Syria. Na hatimaye, mkutano utatazama taarifa za ofisi ya kazi
zilizofanyika katika Beirut, zilizo anzishwa mwaka jana, kwa ajili ya kukusanya
na kusambaza takwimu juu ya kazi za mashirika Katoliki. Wakati wa Mchana mkutano
utatazama masuala ya utendaji wenye ushirikiano kati ya taasisi na vyama mbalimbali
Syria na nchi jirani.
Lengo la mkutano linakwenda sambasamba na njia
zilizochukuliwa miaka miwili iliyopita na Jimbo la Papa , na kama matokeo yake Mkutano
wa Juni 4-5 , 2013 , ulioandaliwa na Baraza la Kipapa , kwa ajili ya kutathmini
kazi zilizo kwisha fanywa na Mashirika Katoliki ya hisani katika mazingira ya mgogoro
wa vita vya Syria ,kwa kuzingatia hali halisi na utambuzi wa vipaumbele kwa siku
zijazo. Syria ni kiini cha tahadhari ya jumuiya ya kimataifa, kutokana na mwendelezo
wa kipeo cha ubinadamu katika mgogoro wake kama matokeo ya vita.