Jeshi la Nigeria katika taarifa yake kwa vyombo vya habari linasema kwamba, limebaini
mahali ambapo wasichana wa shule zaidi ya mia mbili waliotekwa nyara na kikundi cha
Boko Haram mahali walipofichwa na kwamba, kwa sasa Jeshi halina mpango wa kutumia
nguvu ili kuwaokoa wasichana hao ambao wanaendelea kunyanyasika chini ya udhalimu
wa kikundi cha Boko Haram.
Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria amewatia shime
askari wake ili kuendeleza mapambano dhidi ya kikundi cha Boko Haram kinachoendelea
kusababisha maafa makubwa kwa watu na mali zao! Serikali ya Nigeria haitaridhia masharti
yaliyotolewa na Boko Haram ili kuwaachilia wasichana waliotekwa nyara. Mashambulizi
ya Boko Haram nchini Nigeria yameendelea kuongezeka siku hadi siku kiasi cha kuhatarisha
usalama na amani ya watu wengi!