2014-05-28 09:23:30

Kanisa linaishi daima na tumaini la kufanywa upya kwa nguvu ya Roho Mtakatifu - Papa .


Homilia ya Papa Francisko katika Chumba cha Juu!
Baba Mtakatifu Francisko , Jumatatu 26 Mei 14, akiwa mjini Yerusalemu , katika kukamilisha hija yake ya kitume ya siku tatu, alijumuika pamoja na Maaskofu Katoliki wa Nchi Takatifu, kuadhimisha Ibada ya Misa, katika Chumba cha juu gorofani, maarufu kwa jina la Cenacle, ambako Yesu mwenyewe , alifanya karamu ya mwisho akiwa na mitume wake.

Baba Mtakatifu katika homilia yake, alisema, kujumuika kwao katika chumba hicho kwa ajili ya Ibada ya Ekaristi Takatifu, ilikuwa ni zawadi kubwa kutoka kwa Bwana, “hapo , ambapo Yesu alifanya karamu ya mwisho na mitume ; ambapo, baada ya kufufuka Yesu alionekana kati yao; ambapo Roho Mtakatifu alishuka kwa nguvu juu ya Mariamu na kwa Mitume. Hapa Kanisa lilizaliwa, na kuenea kote. Kutoka hapa, uliwekwa nje , mkate uliovunjwa katika mikono yake, majeraha ya Kristo mbele ya macho yake , na roho ya upendo katika moyo wake.

Katika chumba cha juu ghorofani , Yesu aliyefufuka , aliyetumwa na Baba , alimtuma Roho wake , na uwezo uliyowapa nguvu mpya mitume kutoka nje , kwenda kufanya upya uso wa dunia.

Papa alifafanua kwenda nje haina maana ya kusahau. Kwa kanisa kwenda yake nje , ni kulinda na kudumisha kumbukumbu ya yale yaliyojadiliwa kaika Chumba cha juu ambako Roho Mtakatifu alishuka, Roho, Msaidizi anayekumbusha kanisa lililozaliwa hapa, kila neno na kila hatua, na huonyesha maana yake ya kweli.

Chumba cha Juu, Papa anaongeza, kwetu sisi ni kuiona huduma, Yesu alitoa mfano kwa kuosha miguu ya wanafunzi wake. Kuosha miguu ya mtu mwingine kunaashiria, kumkaribisha, kumkubali , kumpenda na kuwa tayari kumhudumia mtu mwingine. Ina maana kuwahudumia maskini, wagonjwa na maluuni.

Chumba cha Juu kinatumbusha , kwa njia ya Ekaristi , na sadaka, kwamba, katika kila adhimisho la Ekaristi Yesu anajitoa mwenyewe kwa ajili yetu kwa Baba, ili kwamba sisi pia tunaweza kuwa na umoja pamoja naye , sadaka kwa Mungu, maisha yetu, kazi zetu, furaha yetu na huzuni zetu ... sadaka kwa kila kitu kama dhabihu ya kiroho .

Chumba cha Juu kinatukumbusha urafiki. "Hakuna tena wa kuitwa mtwana au mtumwa, Yesu alisema kwa mitume wake kumi na wawili - lakini mimi nimewaita rafiki " (Yn 15:15 ). Bwana hutufanya sisi rafiki zake, Yeye anatuonyesha mapenzi ya Mungu, na anatupa nafsi yake sisi. Hii ni sehemu uzuri wa kina wa kuwa Mkristo na , hasa, ya kuwa kuhani, ni urafiki wa ajabu wa Bwana Yesu.

Papa aliendelea kusema, Chumba cha Juu, kinaendelea kutukumbusha ahadi yake ya kurudi kama rafiki, "Mimi nakwenda ... nitakuja tena kuwachukua, ili nilipo mimi nanyi mwepo " (Yn 14:03 ). Yesu hatuachi , wala milele haachani nasi ; yeye anatuandalia sisi makazi katika nyumba ya Baba , anako taka tuwepo pia.

Aidha Chumba cha Juu , , pia kinatukumbusha choyo , na udadisi - "Ni nani msaliti ?" . Sisi wenyewe, tunapaswa kujichunguza dhamiri zetu iwapo tu wasaliti wa ndugu zetu au kwa dharau au kuwahukumu..., na yatupasa kutambua kwamba wakati wowote tunapotenda dhambi, tunamsaliti Yesu.

Chumba cha Juu kinatukumbusha kugawana madaraka na wengine, kuishi kwa udugu, amani miongoni mwetu. Kiasi gani upendo na wema na fadhila vinaonekana kutoka Chumba cha Juu ! Kiasi gani upendo imeenea kutoka hapa, kama mto kutoka chanzo chake, mwanzo kama mkondo wa maji na kisha kupanuka na kutiririka kwa kasi kubwa . Watu wote wa Mungu huchipuka kutokana na chanzo hiki ; na hivyo ni mto mkubwa wa utakatifu wa Kanisa inaendelea ndani yake kutoka moyo wa Kristo , kutoka meza ya Bwana na kwa Roho Mtakatifu.

Mwisho, Chumba cha Juu kinatukumbusha kuzaliwa kwa familia mpya, yaani Kanisa imara la Yesu aliyefufuka ; familia ambayo ina Mama, Bikira Maria. Familia za Kikristo ni watu wa familia hii kubwa , na ndani yake, wao hupata mwanga na nguvu ya kutangaza katika vyombo vya habari juu, habari hii ,mbele ya changamoto na matatizo ya maisha . Watoto wote wa Mungu, kila watu na lugha , wamealikwa, wanaitwa kuitwa kuwa sehemu ya familia hii kubwa, kama kaka na dada na wana na mabinti wa Baba mmoja mbinguni.

kutoka peo hizi , zilizofunuliwa katika Chumba cha Juu , ni upeo wa Bwana Mfufuka na Kanisa lake.
Papa alikamilisha homilia akisema “kutoka hapa Kanisa litasonga mbele kwa msukumo mpya unaovuviwa na pumzi ya uzima ya Roho Mtakatifu” . Wakiwa wamekusanyika katika sala na Mama wa Yesu, kanisa linaishi daima katika matazamio ya kufanywa upya kwa nguvu ya Roho Mtakatifu. Bwana tuna Roho Yako , Bwana , fanya upya uso wa Dunia (cf. Ps 104:30 )”!








All the contents on this site are copyrighted ©.