Useja ni zawadi ya neema kwa Mapadre toka wa Mungu
Papa anasema, useja ni zawadi ya neema kwa Mapadre toka kwa Mungu. Na si imani sadikifu
ya Kanisa , na hivyo mlango ni wazi kwa mabadiliko, iwapo kanisa litapenda kufanya
hivyo. .
Baba Mtakatifu Francisko, alieleza siku ya Jumatatu, wakati akijibu
maswali ya wanahabari akiwa safarini kwa ndege, kurejea Roma , baada ya kukamilisha
hija yake kwa mara ya kwanza katika Nchi Takatifu .Papa alionyesha imani yake kwamba,
Padre Mkatoliki anapaswa kuishi maisha ya useja ingawa si sheria isiyoweza kubadilishwa
na si moja ya kanuni katika mafundisho ya Kanisa.
Alisema Useja ni si “dogma,
na hivyo Kanisa Katoliki halina kizuizi iwapo litapenda kuruhusu Mapdre kuoa kama
wanavyo fanya makuhani katika baadhi ya Makanisa mengine ya Kikristo.
Useja
ni kanuni ya maisha, anayochagua mtu wenyewe kw ahiarai yake, na yeye anaipenda
zaidi na kuichukulia kama ni zawadi ya Mungu kwa Kanisa , na kwa kuwa siyo imani
sadikifu ya Kanisa, mlango daima ni wazi katika mabadiliko . Kanisa hufundisha kwamba,
Padre ni lazima akubali kwa moyo wote na kwa hiari kamili, kuitikia wito wa kujitolea
bila ya kujibakiza kama mchumba wa Kanisa, kwa ajili ya utume wa Kanisa, kimsingi
kuchukua Kanisa kama mke wake na kusaidia kutekeleza lengo lake.
Ingawa
mapokeo ya utamaduni huu, yana historia ya karibia miaka 1,000, bado si sheria sadikifu
ya kanisa, na uwepo wake hauhusiki imani ya kiroho au mafundisho ya Kanisa .Papa alieleza
na kutaja kwamba, kumekuwa na shinikizo la kutaka kufanya mabadiliko na hasa kutokana
na wingi kashfa ya unyanyasaji wa kijinsia zinazo fanywa na baadhi ya Mapadre na
kulidhalilisha kanisa, na utetezi hiari wa useja katika Kanisa.
Kanisa limekuwa
likijitetea kwamba, madhulumu ya ngono kwa watoto , iwe yanafanywa na Mapadre na
watu wengine baki , ni tatizo la kijamii la watu wenye matatizo ya kisaikolojia. Na
kutokana na ukubwa wa tatizo , Kanisa haliwezi kuvumilia makosa yanayofanywa na watu
wenye kasoro hiyo ya kisaikolojia. Na kwamba yeye mwenyewe ana mpango wa kukutana
na wawakilishi wa kundi la waathirika wa unyanyasaji wa ngono mwezi ujao mjini Vatican.
"Kanisa lina uvumilivu sufuri kwa kila kiongozi wa dini anayedhulumu mtoto kigono".
Mpango wa Papa kukutana na wawakilishi wa kundi la waathirika wa madhulumu ya
ngono, baada ya Ibada ya Misa ambayo huongoza katika makazi yake mjini Vatican nyakati
za asubuhi, kunaonyesha mshikamano wake mshikamano binafsi na kanisa kwa ujumla kwa
watu hawa wanaoteswa na kitendo hicho cha aibu, kilichofanywa na Mapadre wabovu.