2014-05-27 14:48:59

Papa karibu tena nyumbani!


Rais Giorgio Napolitano wa Italia amemwandikia Baba Mtakatifu Francisko ujumbe wa matashi mema pamoja na kumkaribisha tena baada ya kuhitimisha hija yake ya kitume Nchi Takatifu. Ni matumaini ya Rais Napolitano kwamba, hija na mwaliko uliotolewa kwa Marais wa Israeli na Palestina wa kukutana na kusali pamoja na Papa Francisko utakuwa ni kikolezo cha matumaini Ukanda wa Mashariki ya Kati, katika mchakato wa kuendeleza majadiliano ya kutafuta haki na amani.

Ni hija ambayo imekoleza majadiliano ya kidini na kiekumene kati ya Wayahudi na Waislam. Ni matumaini ya Rais Giorgio Napolitano kwamba, mwaliko uliotolewa na Papa Francisko utagusa nyoyo za watu wanaotamani kupata amani, maridhiano, upendo na mshikamano!







All the contents on this site are copyrighted ©.