2014-05-27 10:28:24

Hija ya Papa, Salaam kwa Marabbi wawili wa Israel


Jumatatu , Baba Mtakatifu baada ya kutembelea makumbusho ya mauaji ya kinyama dhidi ya Wayahudi ya Yad Vashem, alikutana katika hali ya faragha na Marabbi Wawili wa Israel, Rabbi Yitzhaki Yosef, Rabbi Mkuu wa Sefardita Ashkenazi na Rabbi Daud Lau wa Ashnezi.Viongozi hawa kwanza walikutana katika hali ya faragha.
Wakimpokea Papa, Marabii kwa pamoja walionyesha kufurahia aneno yake makaliya Papa yaliyokemea dhuluma dhidi ya Wayahudi . Na kwa mikono miwili walimkaribisha katika mji wa Yerusalem
Rabbi Yitzhak alisema , Karibu Yerusalemu, mji wenye maana mbili : mji wa kawaida wa Yerusalemu wa hapa duniani , ambako ni nyumbani kwa Wakristo, Wayahudi na Waislamu, na kuna Yerusalemu wa mbinguni, mahali ambapo wanaishi kila mtu wa dini zote za dunia . Na alionyesha tumaini lake kwamba kutoka mahali hapo pataweza kutoa sauti ya amani duniani kote.

Na Papa Francisko alionyesha shukurani zake za dhati kwa makaribisho na wema wao , , na kwa moyo wa udugu waliouonyesha. Na kwamba kwa hakika alijisikia kuwa kati ya ndugu na hasa kuwa kati ya ndugu walio wakubwa kuliko yeye.
Baadaye walikutana sehemu ya hadhara ambako Baba Mtakatifu alitoa shukurani zake kwa marabbi wote na kwa Wakuu wa dini na wageni, Bunge Tukufu , kwa makaribisho yao mazuri katika nchi hii yenye Baraka na Takatifu, na mji huu wa Yerusalemu, mji wa ushindi. Na kwa unyenyekevu na hofu za mji huu,hutoa mfano kama binadamu, kwamba kila mtu aliyeumbwa kwa sura ya Mungu lazima kuishi kwa upendo na kuishi kwa ajili ya udugu.
Mazungumzo kati ya Baba Mtakatifu na Marabbi wa Israel , yalirejea katika mengi na hasa matukio ya hivi karibuni na kanuni nyingine za kiraia na kwa ajili ya dini , moja kwa nyingine. Na kwamba, wanapenda kufanya kazi ya kupambana na dhuluma dhidi ya Wayahudi. Wale wote ambao bado wanafanya maovu katika dunia hii... Papa Francisko alieleza na kuonyesha masikitiko yake kwa tendo lilitokea Brussels. Papa alisisitiza, mapambano haya yatafanikiwa tu , kwa kuheshimu msingi kwa haki na amani ya kudumu , kwa watu wote. Na hivyo Papa alitoa wito wa kukaa pamoja na wawakilishi wa wakuu wa Kanisa na Marabbi kwa ajili ya kuona kwa jinsi gani inawezekana kufanikisha amani ya kudumu duniani . Kisha mapambano dhidi ya ugaidi, Papa alisisitiza kuwa ni jambo muhimu sana kwa ajili ya wote. Papa pia alisisitiza kuwa kuna uhusiano kati ya mtu na Mungu , na hivyo hivyo kuna pia uhusiano kati ya mtu na mtu.
Katika Mkutano huu, Rabbi David Lau - Ashkenazi, aliangalisha juu ya thamani ya maisha, akisema, sisi wote tuna hamu ya kuishi tena maisha ya amani na utulivu. Ni amri ya Mungu kuishi na kusamehe, , kwa sababu sisi sote huomba kwa Mungu msamaha pia kwa watu waliokufa, watoto, wanawake katika mashambulizi , wawe ni Wayahudi, Waislamu na Wakristo, na wengine waliouawa kwa jina la dini. Hivyo hakuna tofauti kati ya moja au nyingine : wao wote wanakumbukwa kwa sababu ya thamani ya maisha ni muhimu sana .
Na Rabbi David Lau , alizungumzia matumaini katika upatikanaji wa juhudi zinazofaa kupambana dhidi ya ugaidi , dhdi ya Uyahudi na kuomba pamoja, ili itokee uwepo wa siku bila vita, wala chuki zaidi, bali ujenzi wa amani na watu wote walio karibu na wale walio mbali na hivyo wote kubarikiwa na sala hii.. Ujumbe huu wa amani , katika urafiki na udugu kwa dunia nzima.







All the contents on this site are copyrighted ©.