2014-05-27 12:00:15

Dumisheni amani na utulivu nchini Malawi!


Mahakama kuu ya Malawi imesema kwamba, Rais Joyce Banda aliyekuwa anagombea nafasi ya Urais kwenye uchaguzi mkuu uliopita hakuwa na mamlaka kikatiba ya kufuta uchaguzi na kuitisha uchaguzi mwingine tena katika kipindi cha siku 90 kutokana na mapungufu makubwa yaliyojitokeza katika mchakato wa uchaguzi huo!

Takwimu zinaonesha kwamba, kuna idadi kubwa ya wapiga kura walioshiriki katika zoezi, ikilinganishwa na namba halisi iliyokuwa kwenye Daftari la wapiga kura!

Viongozi wa kidini nchini Malawi wanawataka wananchi kutulia na kudumisha amani na utulivu wakati huu wakisubiri Tume Huru ya Uchaguzi Malawi kutangaza matokeo ya uchaguzi mkuu baada ya kutokea itilafu kubwa wakati wa kupiga kura nchini humo!







All the contents on this site are copyrighted ©.