2014-05-26 12:32:59

Papa atembelea makumbusho ya Yad Vashem ya Jerusalem


Papa Francisko akiendelea na hija yake Nchi Takatifu , mapema Jumatatu , alitembelea makumbusho ya Wayahudi ya Yad Vashem ya Jerusalem, baada ya kukutana na Mufti Mkuu wa Jerusalem.

Padre Koprowiski, Mkurugenzi Mkuu wa Utangazaji Radio Vatican, ameripoti kwamba, hotuba ya Papa katika ukuta huu, imesisitiza sana unyenyekevu na heshima, kwamba ni nguvu ya kipekee, katika kutoa kujibu kwa vitendo vya kinyama na ukatili , unaoweza kufanya na baadhi ya watu . Na alirejea maneno ya Mtakatifu Yohana Paul II kuwa, unyama huo ni miundo ya dhambi yenye kudhalilisha hadhi ya binadamu, aliyoumbwa nayo na Mungu katika sura na mfano wake , na ni kumkataa Mungu na kujitengenezea badala yake, miungu ya uongo ya kibinadamu.
Na kwamba , katika ukuta huu unao onyesha kukataliwa kwa Mungu , inakuwa ni kumbukumbu inayoonyesha jinsi binadamu anavyoweza kuwa katili asipokuwa na Mungu. .
" Katika kumbukumbu hii ya Mauaji ya kinyama ya Wayahudi , Papa alisema, tunausikia mwangwi wa swali la Mungu kwa binadamu “Adam , uko wapi? (taz. Mwa 3:09 ).
Hili ni swali linalo umiza baba yeyote aliyepoteza mwana . Baba mwenye kujua hatari ya uhuru ; anayejua kuwa mtoto wake anaweza kupotea ..., Baba anayeona mwana wake yuko katika hatari za kuanguka katika shimo kubwa, na kuita kwa nguvu uko wapi . Sauti hii kubwa ya Baba inayoita uko wapi, inasikika katika majanga yote ya uso wa mauaji, ni sauti inayoonya na kututaka turejee kwa baba badala ya kwenda kupotelea katika shimo lisilo na mwisho ... "
Papa akiwa katika ukuta huo, alitolea sala zake kwa kumlilia Bwana wa haki, kwamba, wakiwa wamaegubikwa na uso wa haya na aibu kwa unyama huu, wanamwinamia Mungu na kuomba huruma yake. Aliomba neemaya Bwana iwezeshe binadamu wote kuenea aibu, moyo wa kufanya maasi ya kijinga, kudharau na kuharibu mwili wa binadamu , kama vile ni tope lisilo kuwa na pumzi ya maisha toka kwako Mungu.Papa alipaza sauti yake akisema “ Kamwe tena , Bwana , kamwe tena ! Jambo hili lisitendeke. Adam, uko wapi , sauti yako inatuita?" .

Na kwamba wakiwa katika makumbusho hayo, wanamwita Bwana, kwa aibu ya mtu huyo , aliye umbwa kwa sura na na mfano wa Mungu ,aliyepata nguvu za kufanya maovu hayo .Aliomba Bwana wa huruma, awakumbuke wote katika huruma yake. Sala ya Papa Francisko ilimalizia.







All the contents on this site are copyrighted ©.