Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican inapenda kukushirikisha utajiri wa tafakari ya
Neno la Mungu, Jumapili ya Vi ya Kipindi cha Pasaka inayomwonesha Roho Mtakatifu kuwa
kweli ni kocha na mwalimu wa maisha ya kiroho! Kazi kwako!
Katika Injili NENO
KUPENDA/PENDO linatawala – hivi unajisikiaje unapoambiwa nakupenda au unapohisi kuwa
unapendwa? Hakika kupenda kunawajibisha - tamko hilo lasubiri jibu. Wengi wetu twafahamu
fika jinsi ilivyo vigumu kupenda upeo/kweli. Upendo unadai matendo. Kinachofuata ni
wajibu.
Ndicho kinachoonekana katika masomo yetu ya leo = kutii amri na
kuabudu. Ndiyo maana Yesu anaweza kusema mkinipenda mtazishika amri zangu. Mtakatifu
Tomas wa Akwino - sheria za Mungu ni nyepesi kwa wapendao na mzigo kwa wasiopenda.
1 Jan 4,8 yeye asiyependa hakumjua Mungu kwa maana Mungu ni upendo -hivyo ili
kupenda vizuri ni lazima kumjua Mungu sababu yeye ni PENDO. Mapendo ya kweli yadai
sadaka. Ili kushika amri au sheria inavyotakiwa yahitaji sadaka kubwa na inayodai
utumishi.
Mt Agustino anapotafakari juu ya upendo wa Mungu anasema - umegusa
mioyo yetu kwa pinde za upendo wako na akili zetu kwa mishale ya neno lako.
Baada
ya utangulizi na kusikia masomo kinachotakiwa na kuweka katika matendo. Ndicho kinachoonekana
katika masomo yetu na baada ya kuelewa kuishi.
Katika somo la 1 - Roho Mtakatifu
anafanya kazi ndani ya Petro. Ubatizo wetu unatuwajibisha. Sisi tumebatizwa kwa jina
la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Tumezamishwa ndani yake Mungu, katika Utatu Mtakatifu.
Sisi tunashiriki ile asili ya Kimungu. Hatuitwi kwa jina linguine ila ni watoto wa
Mungu na ndivyo tulivyo.
Katika somo la 2 - Twaona wingi wa neema ya tendo
la Mungu la kuokoa na hitaji la utayari wa mkristo. Petro anasema mpokeeni Kristo,
na ondoeni roho ya woga. Halafu Petro asema - kuweni na uwezo wa kuelezea imani yenu
- ni kwa ajili yake twafanya mambo haya. Imani yetu na maisha yetu - msingi wake ni
Kristo aliyekufa na akafufuka. Sababu ya matumaini yetu – inaonekana katika ukuaji
wa ufalme wa Mungu na kumpenda Mungu. Matumaini yetu ni ufalme wa Mungu, utukufu wa
Mungu, upendo wake, ujio wa mbingu mpya na nchi mpya, ujio wa ufalme wa haki na amani.
Tukumbuke kuwa Roho wa Mungu hushuhudiwa na anatakiwa aonekane katika maisha yetu
ya kila siku. Gal. 5:22-23 – lakini matokeo ya Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu,
hisani, ukarimu, uaminifu, upole na kiasi.
Katika Injili - Baba atampa Roho
Mtakatifu
Hivyo tunamwona Baba anayependa kwa njia ya Roho Mtakatifu na Mwanaye.
Hivyo
Petro na Yohani wanaondoka kwenda kutangaza habari njema na wale waliobatizwa na Filipi
wakawekewa mikono na kupokea Roho Mtakatifu. Na hapo yaonekana mwanzo wa mitume kwenda
kuhubiri habari njema duniani.
Ndiyo maana sisi tumeitwa kuitikia huu mwito
– kuishi kadiri ya amri za Mungu. Mambo haya mawili hayatengani - upendo na utii.
Hii ndiyo kazi kuu ya Roho Mtakatifu - Huyu Roho anayepelekwa atawezesha udumifu
wetu katika maisha ya ukristo.
Huyo Roho = wakili, mfariji, mshauri msaidizi.
Kigiriki
ni yule anayesimama kando ya mteja na kwa lugha ya kisheria ni mwanasheria, wakili.
Pengine lugha ya siku hizi ni tungesema ni kocha, mwalimu. Roho Mtakatifu yupo nasi
pamoja na anatuongoza, sahihisha.
Hakuna mwanadamu aliye mkamilifu Mganga
hajigangi Hata wachezaji maarufu – mpira, mbio n.k wanahitaji mwalimu.
Peke
yetu bila Mungu hatuwezi kitu. Watu wengi huamini na kudhani kuwa hawana haja ya msaada,
ushauri, mawaidha kushirikiana na wengine n.k. Je ni kweli.
Katika mojawapo
ya mafundisho ya Papa Benedict XVI kabla ya uteuzi – akiongea dhidi ya watu wanaoishi
bila mwelekeo - wanaodhani kuwa hawahitaji Mungu wa mwanadamu mwenzio – anasema matokeo
yake huwa kinyume cha wote.
Ni kwa jinsi gani tunaweza kupokea hiyo zawadi
ya Mungu? Huyo Roho Mtakatifu?
Ni katika kuishi amri ya mapendo kwa Mungu na
jirani Yoh 14,15-16
Baada ya kupaa Bwana mitume na wanawake walienda chumba
cha juu – wakisali na kusubiri - Mdo 1,14 hatuna budi nasi kufanya hivyo. Kipindi
kati ya kupaa Bwana na Pentekoste ni kipindi cha sala na subira - tukijiandaa kumpokea
Roho mtakatifu. Sote tunaalikwa kufanya hivyo - tunamhitaji mwalimu, kiongozi n.k
- leo kama iliyokuwa miaka 2000 iliyopita.