2014-05-24 11:50:03

Papa Francisko anaomba sala yako!


Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii, anawaomba kumsindikiza kwa njia ya sala katika hija yake ya kitume huko Nchi Takatifu.

Baba Mtakatifu Jumamosi tarehe 24 anatembelea Amman nchini Yordan, Jumapili tarehe 25 Mei 2014 atatembelea Palestina na kwa namna ya pekee mjini Bethelehemu na Jumapili jioni, atakuwa Israeli na kilele cha hija hii ya kitume ni mjini Yerusalemu atakapokutana na kusali pamoja na Patriaki Bartolomeo wa kwanza kama sehemu ya maadhimisho ya Jubilee ya Miaka 50 tangu Papa Paulo VI alipokutana na Patriaki Anathegoras wa Yerusalem.







All the contents on this site are copyrighted ©.