2014-05-23 12:15:49

Papa Francisko ajikabidhi chini ya ulinzi wa Bikira Maria!


Baba Mtakatifu Francisko Ijumaa, tarehe 23 Mei 2014 asubuhi na mapema, aliondoka kutoka mjini Vatican na kwenda kusali kwenye Kanisa kuu la Bikira Maria mkuu lililoko mjini Roma, kuomba ulinzi na tunza ya Bikira Maria kabla ya kuanza hija yake ya kichungaji Nchi Takatifu itakayomwezesha kutembelea: Yordan, Palestina na Israeli kama sehemu ya maadhimisho ya Jubilee ya Miaka 50 tangu Papa Paulo VI alipokutana, akazungumza na kusali na Patriaki Anathegoras wa Yerusalemu.

Baba Mtakatifu Francisko alipokuwa anatangaza hija hii ya kitume aliwaambia waamini waliokuwa kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican kwamba, hija hii itafikia kilele chake wakati viongozi wawakilishi wa Makanisa watakaposali kwa pamoja kwenye Kaburi Takatifu, mwendelezo wa mchakato wa majadiliano ya kiekumene, ili wote wawe wamoja!







All the contents on this site are copyrighted ©.