Watoto wanaoishi katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma iliyoko Kaskazini Mashariki wa
Kenya wanakabiliana na mazingira hatarishi kwa usalama wa maisha na makuzi yao kwa
sasa na kwa siku za usoni. Kuna watoto wanaokimbia vita na kinzani za kijamii kutoka
kusini mwa Sudan na kuwasili kambini hapo pasi na usimamizi wa wazazi wala walezi
wao. Kundi hili la watoto linahitaji huduma makini zaidi ili kukabiliana na mazingira
magumu kwa sasa.
Taarifa ya Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa
inaonesha kwamba, walau asilimia 71% ya wakimbizi wote duniani ni watoto wenye umri
chini ya miaka 18. Idadi ya wakimbizi wanaofika kila siku inazidi kuongezeka kiasi
kwamba, huduma msingi zinazotolewa kwa wakimbizi hawa zinasuasua.