Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi, tarehe 22 Mei 2014 amewapangia Makardinali wapya
waliosimikwa kwenye Ibada iliyofanyika hapo tarehe 22 Februari 2014 Mabaraza ya Kipapa
watakayoshiriki kama wajumbe. Kutoka Barani Afrika Makardinali wamepangiwa Mabaraza
ya Kipapa yafuatayo:
1. Kardinali Philippe Nakellentuba Ouèdraogo, Askofu mkuu
wa Jimbo kuu la Ouagadougou atakuwa mjumbe wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa
Watu pamoja na Baraza la Kipapa la Majadiliano ya kidini.
2. Kardinali Jean
-Pierre Kutwa, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Abijan, Pwani ya Pembe atakuwa mjumbe wa
Baraza la Kipapa la Mashirika ya Kitawa na Kazi za kitume. Ameteuliwa pia kuwa mjumbe
wa Baraza la Kipapa la Walei pamoja na Baraza la Kipapa la Haki na Amani.