Mafaniko ya uchumi ni lazima kuwiana na mipango ya elimu
Katika nyakati ambamo mna mwelekeo wa vijana wengi wa Afrika kuhamia mijini kuliko
kubaki vijijini , ni muhimu kwa viongozi wa Afrika kuwa na mipango mizuri inayokidhi
mahitaji ya makazi mapya ikiwemo , miundo mbinu na uzalishaji wa chakula kwa ajili
ya kasi ya ongezeko la watu mijini, na pia kujali maendeleo na usalama wa wale wanaobaki
vijijini . Ni makala ya Makhtar Diop, katika jarida la Benki ya Dunia, toleo la Mei
2014.
Amesema, pamoja na taarifa za uvumbuzi mpya wa mafuta, gesi na madini
vinavyosikika kila mwezi , Afrika inahitaji kuwa na uwezo wa dondoo katika soko
la dunia, na uwekezaji katika mapato mpya, hasa katika viwango vya juu vya elimu,
afya , na vipaumbele vingine muhimu katika maendeleo endelevu.
Mwandishi
ameeleza kwa kuangalisha katika ukweli kwamba, Afrika katika kipindi cha muongo
mmoja uliopita imekuwa na mafanikio ya kipekee katika ukuaji wa uchumi,lakini bado
Waafrika wengi wanaishi katika hali ngumu na umaskini wa kukithiri. Katika kipindi
hicho uchumi ulikua katika kiwango cha wastani wa asilimia 4.5 kwa mwaka, kutoka
na usimamizi makini katika uchumi . Na sasa, inakuwa ni muhimu kudumisha maendeleo
hayo hasa katika kuwa na uchumi wenye kuwezesha kufuta umaskini wa kukithiri na
kufanikisha elimu kwa watu wote wa bara la Afrika.
Na kwa kadri kunavyokuwa
na msukumo mpya wa nguvu kwa watu kuhamia mijini, inalazimu pia kushughulikia kwa
namna ya kipekee mahitaji mapya kwa ajili ya makazi , miundombinu, na uzalishaji
wa kilimo kulisha wakazi wa mijini, na kuwa na uhakika wa chakula kwa maeneo ya vijijini
pia.
Aidha ni muhimu kujali mabadiliko ya tabia nchi na mazingira , ambayo
Afrika imeathiriwa kwa uwepo wa maafa kama ukame wa kukithiri, mafuriko na kupanda
kwa viwango vya bahari ambavyo vimeleta a hasara za kiuchumi na ugumu wa maisha.
Wakati
huo huo, changamoto hizi pia zichukuliwe kama fursa kwa ajili ya utafiti wa pamoja
utakaowezesha wanasayansi duniani kote duniani kutenda kwa mshikamano na umoja kwa
manufaa ya dunia nzima . Kwa namna hiyohiyo pia ni muhimu katika kuwa na ushirikiano
sawia katika utafiti kati ya wanasayansi wa Afrika na nje ya nchi, hasa kwa ajili
ya tiba, dawa, viumbe hai, kilimo cha umwagiliaji , uhandisi , madini na maeneo
mengine.
Lakini mafanikio ya umoja katika utafiti inapaswa kuwa ni changamoto
ya kusisimua barani iwapo kutafanyika masahihisho katika kosa la muda mrefu la kukosa
usawa na uwiano katika mfumo wa elimu. Leo, hisa za wahitimu katika elimu ya juu
bado zimelemea katika masomo ya sanaa na sayansi ya jamii, wakati sehemu ya wanafunzi
katika sayansi, teknolojia, uhandisi, na hisabati , umebaki katika wastani wa chini
ya asilimia 25. Na mbaya zaidi, kiwango kinashuka zaidi katika uwepo wa wanawake katika
masomo ya sayansi na teknolojia. Hata hivyo pamoja na hayo, shukrani kwa maendeleo
ya hivi karibuni ya elimu kwa wote , juhudi zilizofanikisha watoto wengi kuandikishwa
katika mfumo wa elimu ya msingi barani Afrika, zaidi na zaidi ya wanafunzi wanakamilisha
elimu ya msingi na sekondari . Juhudi hizi zinaleta matumaini kwamba, kizazi kipya
cha vijana Waafrika, kitakuwa na elimu na ujuzi wa kisasa na maarifa yanayohitajika
kupata ufumbuzi dhidi ya changamoto ya Afrika.