2014-05-19 15:13:50

Mfalme wa Bahrein akutana na kuzungumza na Papa mjini Vatican


Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu tarehe 19 Mei 2014 amekutana na kuzungumza na Mfalme Hamad Bin Isa Al Khalifa wa Bahrein ambaye baadaye alibahatika kuzungumza na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican aliyekuwa ameambatana na Askofu mkuu Dominique Mamberti, Katibu mkuu wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican.

Viongozi hawa wamejadiliana masuala muhimu katika maisha ya mwanadamu kwa kujikita zaidi katika mchakato wa amani na utulivu huko Mashariki ya Kati pamoja na kukazia majadiliano yatakayoihusisha Jamii.

Kwa pamoja wamepongeza mchango unaotolewa na Wakristo huko Bahrein, lakini kwa namna ya pekee kabisa Kanisa Katoliki katika huduma kwa wananchi.







All the contents on this site are copyrighted ©.