2014-05-16 07:28:15

Macho na masikio yetu yako Jimbo kuu la Songea!


Askofu mkuu mteule Damian Dennis Dallu wa Jimbo kuu la Songea, Tanzania aliyeteuliwa hivi karibuni na Baba Mtakatifu Francisko anatarajiwa kusimikwa rasmi kama kiongozi mkuu wa Jimbo kuu la Songea, Jumapili tarehe 18 Mei 2014. RealAudioMP3

Akizungumza na Radio Vatican, Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania na aliyekuwa msimamizi wa kitume wa Jimbo kuu la Songea anasema, Familia ya Mungu Jimbo kuu la Songea, imejipanga vyema kumkaribisha Askofu mkuu Dallu ambaye hadi uteuzi wake alikuwa ni Askofu wa Jimbo la Geita.

Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania anaiomba Familia ya Mungu Jimbo kuu la Songea kumpokea Askofu mkuu Dallu kwa mikono miwili na kumpatia ushirikiano wa dhati, ili kwa pamoja waweze kushikamana kulijenga na kuliendeleza Jimbo kuu la Songea kadiri ya mapenzi Mungu.







All the contents on this site are copyrighted ©.