2014-05-15 11:45:06

Papa kutembelea Madhabahu ya "Divino Amore" wakati mwingine, lakini si Jumapili ijayo!


Padre Federico Lombardi, msemaji mkuu wa Vatican anasema kwamba, Baba Mtakatifu Francisko ameahirisha ziara yake ya kutembelea kwenye Madhabahu ya Bikira Maria wa "Divino Amore" yaliyoko mjini Roma hadi hapo itakapotangazwa tena.

Baba Mtakatifu alikuwa anatarajiwa jumapili ijayo kutembelea na kusali kwenye Madhabahu ya "Divino Amore" nyakati za jioni, lakini kwa sasa ziara hii imefutwa ili kumpatia nafasi Baba Mtakatifu kujiandaa zaidi kwa ajili ya hija yake ya kichungaji, anayotarajia kuifanya huko Nchi Takatifu kuanzia tarehe 24 hadi tarehe 26 Mei 2014, ikiongozwa na kauli mbiu, wote wawe wamoja!







All the contents on this site are copyrighted ©.