2014-05-14 15:08:29

Utu na heshima ya binadamu!


Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya Katekesi yake siku ya Jumatano, tarehe 14 Mei 2014 amesali kwa namna ya pekee kwa ajili ya kuwaombea wachimba mgodi huko Soma, nchini Uturuki, waliofariki dunia baada ya kufunikwa na kifusi na bado kuna kundi kubwa la wachimba mgodi ambalo bado halijukilani liliko. Baba Mtakatifu anawaombea wote waliofariki dunia pamoja na familia zao, ili waweze kupata faraja kutoka kwa Mwenyezi Mungu, mwingi wa huruma na mapendo.

Baba Mtakatifu Francisko pia amewakumbuka wahamiaji na wakimbizi waliofariki maji kwenye Bahari ya Mediterania, wakati wakijaribu kuvuka kutoka Afrika kwenda Ulaya. Baba Mtakatifu anasema, haki msingi za binadamu zinapaswa kupewa kipaumbele cha kwanza pamoja na Jumuiya ya Kimataifa kuunganisha nguvu zake kwa ajili ya kuokoa maisha ya watu wanaofariki dunia huko Baharini.







All the contents on this site are copyrighted ©.