2014-05-13 11:33:07

Kardinali Marco Cè amefariki dunia


Familia ya Mungu Jimbo kuu la Venezia inatangaza kifo cha Kardinali Marco Cè, Patriaki mstaafu wa Jimbo kuu la Venezia kilichotokea, tarehe 12 Mei 2014 kwenye Hospitali ya Watakatifu Yohane na Paulo mjini Venezia, alikokuwa amelazwa tangu tarehe 19 Machi 2014 baada ya kuvunjika mguu. Tarehe 13 Aprili 2014 akapewa Sakramenti ya Mpako wa Wagonjwa.

Kardinali Cè alizaliwa tarehe 8 Julai 1925 Jimboni Cremona. Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi, akapadrishwa kunako tarehe 27 Machi 1948. Tarehe 22 Aprili 1970 akateuliwa na Mtumishi wa Mungu Papa Paulo VI kuwa Askofu msaidizi wa Jimbo kuu la Bologna. Tarehe 7 Desemba 1978 akateuliwa na Mtakatifu Yohane Paulo II kuwa Patriaki wa Venezia.

Tarehe 30 Juni 1979 akateuliwa kuwa Kardinali wa Venezia ambako amewatumikia Watu wa Mungu kwa kipindi cha miaka 23 na kung'atuka kutoka madarakani hapo tarehe 5 Januari 2002.







All the contents on this site are copyrighted ©.